Klabu ya Italy Napoli imemteuwa Rafael Benitez, Miaka 53 kuwa Meneja mpya wa klubu hiyo ambayo katika Msimu huu imeshika Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Juventus.
Msimu ujao wa 2013/14, Napoli itacheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
katika suala nzima la benitez kutua hapo ni kutokana na aliyekuwa Meneja wa club hiyo Walter Mazzarri, alitangazwa kuiacha Napoli na kuhamia Inter Milan.
Uteuzi huo wa Benitez ulithibitishwa na Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis ambae alimsifia Benitez na kumwita Kocha mwenye ujuzi wa Kimataifa.
aidha Benitez ndio kwanza amemaliza Kibarua cha kuwa Meneja wa muda Klabuni Chelsea na, Wiki mbili zilizopita, hapo Mei 15, aliiwezesha Chelsea kutwaa Kombe la EUROPA LIGI baada ya kuichapa Benfica Bao 2-1 kwenye Fainali.
hata hivyo Benitez aliteuliwa Meneja wa muda wa Chelsea Novemba Mwaka jana baada ya kufukuzwa Roberto Di Matteo.