WAKALA
wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Robert Lewandowski
amesema kuna uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kujiunga na mabingwa
wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Bayern Munich. Hata
hivyo, wakala huyoaitwaye Cezary Kucharski aliiambia luninga moja
nchini Ujerumani kwamba Bayern bado hawajafikia makubaliano ya mambo
binafsi ya nyota huyo wa kimataifa wa Poland. Wakala
huyo aliendelea kusema kuwa wao wako tayari lakini badi hawajasaini
chochote kwasababu klabu nayo inatakiwa iafiki makubaliano hayo. Bayern
ambao ni mabingwa wapya wa Ujerumani tayari wamemnyakuwa kiungo wa
Dortmund Mario Gotze mwenye umri wa miaka 20 kwa ada ya euro milioni 37.