MMOJA APOTEZA MAISHA KATIKAMICHUANO YA LANGALANGA YA CANADIAN.
MASHINDANO ya langalanga
ya Canadian Grand Prix jana yalimalizika kwa Majonzi makubwa baada ya
mmoja wa wafanyakazi mwenye umri wa miaka 38 kufariki baada ya
kukanyagwa na winji. Ajali
hiyo ilitokea wakati gari la dereva Esteban Gutierrez wa timu ya Sauber
lilipokuwa likiondolewa barabara za Montreal baada ya kupata ajali.
Mashuhuda
wanasema wakati winji hilo likijaribu kuliondoa gari hilo ndipo
mfanyakazi huyo aliangusha radio yake na wakati akiiokota ndipo
alipokanyagwa kwasababu dereva wa winji hakumuona. Katika
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter Gutierrez alituma salamu
zake za rambirambi kwa familia ya mfanyakazi huyo kwa kumpoteza mtu wao
karibu. Mbali na
Gutierrez madereva wengine waliotoa rambirambi zao ni pamoja na
Sebastian Vettel wa Red Bull aliyeshinda mbio hizo pamoja na Fernando
Alonso wa Ferrari aliyeshika nafasi ya pili. Hilo
ni tukio la pili kutokea katika mashindano hayo kwani mwaka jana katika
michuano ya Grand Prix ya Italia mfanyakazi wa kujitolea wa zimamoto
Paolo Ghislimberti alifariki kutoka na amejraha aliyopata kichwani na
kifuani baada ya kupigwa na tairi lililochomoka kutoka katika gari la
Heinz-Harald Frentzen wa timu ya Jordan.