KLABU ya Al Ahli ya Saudi
Arabia imethibitisha na kuweka wazi kuwa imemteua Vitor Pereira kuwa kocha mpya wa klabu
hiyo baada kocha huyo kuondoka Porto mwishoni mwa msimu huu. Pereira
ameifundisha Porto kwa kipindi cha misimu miwili baada ya kuchukua
nafasi ya Andre Villas-Boas Juni mwaka 2011 na kuisadia klabu hiyo
kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini Ureno. Katika taarifa
iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo, Pereira mwenye umri wa miaka
44 atajiunga rasmi na klabu hiyo Juni 27 kabla ya kuiandaa timu kwa
ajili ya msimu ujao siku mbili baadae. Pia zimekuwepo taarifa kuwa
atatua katika klabu hiyo na wasaidizi wake wa watatu kutoka Ureno kwa
ajili ya kuimarisha benchi lake la ufundi.