Monday, June 3, 2013

WENGER AKIRI KUWA NA NIA YA KUMSAJILI ROONEY WA MANCHESTER UNITED"

KOCHA wa klabu ya Arsenal The gunners, Arsene Wenger amekiri kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney. Wenger amekuwa akifuatilia nyendo za nyota huyo aliyeomba kuondoka mwishoni mwa msimu huu huku klabu za Chelsea na Paris Saint-Germain nazo pia zikionyesha nia ya kutaka saini ya mchezaji huyo. Akihojiwa na luninga ya Al Jazeera, Wenger amesema Rooney ni aina ya mchezaji ambaye timu yoyote kubwa duniani itahitaji huduma yake ndio maana wanafuatilia nyendo zake kama akishindwa kubakia United watajaribu kumsajili. Arsenal inategemewa kutumia kiasi cha paundi milioni 80 kwa ajili ya usajili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi huku wakijipanga kusaini mkataba mpya wa jezi zao na kampuni ya Puma. Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka jana, PSG wao wamepanga kumpa Rooney mshahara wa paundi milioni 350,000 kwa wiki baada ya kukatwa kodi ili kumshawishi nyota huyo kwenda Ufaransa.