Rais wa Real madrid FLORENTINO Perez
amechaguliwa kwa kipindi kingine tena katika nafasi ya urais wa klabu hiyo
katika mkutano wa uchaguzi uliofanyika mapema leo. mchakato wa uteuzi wa majina lilimalizika Jumamosi usiku wakati muda wa kuchukua
fomu za kugombea nafasi hiyo ulipomalizika bila ya kutokea mgombea
yoyote wa kushindana na Perez. Kutokana
na hilo bodi ya uchaguzi ya klabu hiyo ilimpitisha na kumpigia kura
kama mgombea pekee kwenye uchaguzi huo na baadae kutoa taarifa kupitia
katika mtandao wake. Perez mweye umri wa miaka 66 ameiongoza klabu hiyo toka mwaka 2000.