KLABU ya Chelsea ya
Uingereza, imefanikiwa kunasa saini ya golikipa wa kimataifa wa
Australia Mark Schwarzer kwa usajili huru mpaka mwishoni mwa michuano ya
Kombe la Dunia mwakani. Schwarzer
mwenye umri wa miaka 40, amecheza soka kwa muda wa miaka 15 nchini
Uingereza katika vilabu vya Bradford City, Middlesbrough na Fulham. Msimu
uliopita golikipa huyo alitajwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka nje ya
Uingereza kucheza mechi 500 katika Ligi Kuu nchini humo. Akihojiwa
mara baada ya kukamilisha usajili wake, Schwarzer amesema ni heshima
kubwa kwake kuiwakilisha klabu yenye hadi ya juu duniani kama Chelsea na
anamatumaini ya kufanya vyema akiwa hapo.