Club
ya Bayern Munich ya ujerumani imefanikiwa kutoa wachezaji wa nne walioteuliwa katika orodha ya wachezaji 10 na
Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kugombea tuzo ya mchezaji bora wa
bara hilo kwa msimu wa 2012-2013. Wachezaji
hao ni Franck Ribery, Thomas Mueller, Arjen Robben na Bastian
Schwainsteiger ambao wote walikuwemo katika kikosi cha Bayern ambacho
kilifanikiwa kunyakuwa mataji matatu msimu uliopita. Mbali
na hao wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni mchezaji bora wa mwaka
katika Ligi Kuu nchini Uingereza, Gareth Bale pamoja na mfungaji bora wa
ligi hiyo Robin van Persie huku Lionel Messi na Cristiano Ronaldo
wakiwa wachezaji pekee kutoka La Liga ya nchini Hispania kwenye orodha
hiyo. Hii itakuwa
ni mara ya tatu kufanyika sherehe za tuzo hizo ambapo mwaka 2011 Messi
ndiye aliyeshinda huku mchezaji mwenzake wa Barcelona Andres Iniesta
akishinda tuzo hiyo mwaka jana. Wachezaji
wengine ni Mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG,
Zlatan Ibrahimovic na Robert Lewandowski anayekipiga Borussia Dortmund
ambapo orodha ya mwisho ya wachezaji watatu itatajwa Agosti 6 kabla ya
sherehe za kumjua mshindi ambazo zitafanyika wakati wa upangaji wa
ratiba ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Agosti 29 mwaka huu jijini Monaco.