KOCHA wa klabu ya
Manchester United, David Moyes kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa
Wayne Rooney hawezi kuuzwa baada ya Chelsea kudai kuwa mshambuliaji wa
kimataifa wa Uingereza ndio chaguo lao katika kipindi hiki cha usajili
majira ya kiangazi. Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Sydney, Australia katika ziara yao ya
kujiandaa na msimu mpya, Moyes amesema msimamo wa klabu kuhusiana na
mustakabali wa nyota huyo bado haujabadilika.
Akitupiwa
swali lingine kuhusiana na suala ofa iliyotolewa na United kwa ajili ya
kumnasa kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas, Moyes amesema hajajua suala
hilo linaendeleaje lakini anategemea katika siku mbili zijazo
atafahamishwa na maofisa wa United maendeleo yake. Ofa
ya kwanza ya meneja mpya wa Chelsea Jose Mourinho kutaka kumsajili
nyota huyo tayari imekataliwa na United lakini klabu hiyo bado
imeendelea kufuatilia nyendo za nyota huyo.
