Beki mahiri mwenye nguvu na
kasi Mbuyi Twite ataikosa mechi ya keshokutwa wakati Yanga itakapowavaa URA,
timu inayomilikiwa na kampuni ya watoza kodi ya mapato ya Uganda.
URA itakuwa nchini kucheza
mechi mbili za kirafiki, ikianza na Simba kesho kabla ya kuivaa Yanga,
keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Twite amesema ataikosa
mechi hiyo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti ingawa amekuwa akifanya
mazoezi taratibu.
Awali Yanga ilikuwa icheze
mechi ya kirafiki dhidi ya 3 Pillars ya Nigeria, jana lakini ikagundulika timmu
hiyo ilikuwa bagumashi kupita kiasi.
TFF ikapoga stop mchezo huo
kwa kuwa Wanigeria hao walikuwa wameokotana lakini walitaka kucheza na mabingwa
wa Tanzania.