KATIBU MKUU wa TFF, Angetilie
Osiah, amesema wamefuta Mechi za Klabu kutoka Nigeria, FC 3 Pillars, walizokuwa
wacheze Nchini baada ya Shirikisho la Soka la Nigeria, NFF, kusema haijui
lolote kuhusu Timu hiyo na Ziara yake.
Kwa mujibu wa Osiah, imebidi TFF
waifute Ziara hiyo ya Klabu hiyo ya Nigeria kwa sababu Kanuni za FIFA
haziruhusu Timu kucheza nje ya Nchi zao bila Kibali toka kwa Mamlaka ya Soka ya
Nchini kwao.
Vile vile TFF imesema FC 3
Pillars haijapandishwa Daraja kucheza Ligi Kuu ya Nigeria, NPL [Nigeria Premier
League] kama vile tamko la Waandaaji wa Ziara yao Nchini, SportLink
International, walivyodai kwenye Matangazo yao.
Jana FC 3 Pillars ilikuwa icheze
na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na pia Timu hiyo
ilipangiwa kucheza na Coastal Union na Mbeya City, ambayo Msimu huu unaokuja
itacheza Ligi Kuu Vodacom baada ya kupanda Daraja.
Licha ya kuifuta Ziara ya FC 3
Pillars, pia Katibu Mkuu wa TFF, Angetiilie Osiah, alibainisha kuwa hata hao
Waandaaji, SportLink International, hawajasaliwa na FIFA kwa ajili ya kuandaa
Mechi za Kimataifa kama vile taratibu zinavyotaka.
Akiongeza, Osiah alivitaka Vyama
vya Soka vya Mikoa viwe waangalifu wasidanganywe na Wajanja wanaoleta Timu toka
nje bila ya kufuata taratibu zilizowekwa.