Mshambuliaji Didier
Kavumbagu mchana wa leo amesaini mkataba
wa mwaka mmoja na mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu
ya Azam fc.

Maganga amesema Kavumbagu
tumem
alizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, hivyo basi tutakuwa
nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano
ya klabu bingwa ya Afrika.
Kavumbagu ambae ni Mshambuliaji mahiri na nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino
Azam baada ya Uongozi wa Yanga kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya
ule wa miaka miwili kumalizika.
Maganga amesema kuwa lengo la kuanza usaji mapema ni kuweka mipango mathubuti katika kuhakikisha azam fc inakuwa timu bora na kuweza kukiweka imara kikosi hicho katika msimu ujao pamoja na ligi ya mabingwa barani africa