Friday, April 25, 2014

MAJARIBIO YA AZAM ACADEMI YASOGEZWA MBELE".

MAJARIBIO ya kusaka vipaji vya kujiunga na akademi ya Azam FC ambayo hufanyika kila tarehe ya mwanzo ya mwezi, hayatakuwepo kwa miezi ya Mei na Juni, mwaka huu.
Kocha Mkuu wa Azam Academy, Vivek Nagul raia wa India amesema majaribio yafuatayo yatafanyika Julai 1 mwaka huu kuanzia Saa 12.30 asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Vivek ameomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na amewataka vijana wenye ndoto za kujiunga na akademi hiyo kujitokeza Julai 1 kujaribu bahati yao. “Wazazi pia, ambao wana ndoto za kuwaleta vijana wao hapa, tunapenda kuwaambia nafasi nyingine kwao ni Julai 1, wanakaribishwa,”alisema.