Friday, April 25, 2014

MIAKA 20 WA KENYA WATUA KUIVAA NGORONGORO HEROES

TIMU ya vijana ya Kenya inatarajiwa kuwasili nchini leo (Aprili 25 mwaka huu) saa 1 usiku tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanz

ania (Ngorongoro Heroes).
Mechi hiyo ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 itachezwa Jumapili (Aprili 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 na sh. 5,000.

Kenya na Ngorongoro Heroes zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa Machakos wiki tatu zilizopita.
Mshindi baada ya mechi ya marudiano atacheza na Nigeria katika raundi itakayofuata.
Ngorongoro Heroes inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo chini ya Kocha John Simkoko. Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana wakati Kamishna ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.