KOCHA Tim Sherwood amefukuzwa
Tottenham Hotspur kiasi cha miezi sita tang aanze kazi White Hart Lane.
Sherwood alirithi mikoba ya Andre
Villas-Boas Desemba kwa Mkataba wa miezi 18, lakini ameshindwa kuingia katika
msimu wa pili na klabu hiyo.
Tetesi za kuondolewa kwa Sherwood
zilianza mwezi uliopita, na hatimaye Mwenyekiti Daniel Levy kutafuta mtu
mwingine mwafaka zaidi.
Sherwood ameshinda mechi 14
kati ya 28 akiwa kazini, akitoa safe nne na kufungwa 10, Spurs ikimaliza
katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi 10 na Arsenal
iliyomaliza nafasi ya nne.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 45
anaweza kupewa ofa mara moja kurejea kurejea klabu ya Daraja la
kwanza, Brighton baada ya Oscar Garcia kujiuzulu baada ya kufungwa katika mechi
ya Nusu Fainali ya mchujo dhidi ya Derby.