Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali,
amewapa somo wanachama wa klabu hiyo kuwa makini katika kuelekea kwenye
Uchaguzi huo.
Akizungumzia hilo jijini Dar es Salaam, Dalali alisema kuwa sio wote
wanastahili ku
wa viongozi wa klabu hiyo kongwe ambayo kwa sasa imepoteza
hadhi yake.
Alisema alipokuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, aliweza kuwaunganisha
wana Simba, hivyo kunastahili kiongozi mwingine mwenye mfano wake.
“Hii Simba sasa imepoteza hadhi na heshima yake katika nyanja ya
soka, hivyo lazima apatikane kiongozi imara na mwenye uwezo wa
kuitumikia usiku na mchana.
“Tunahitaji kupata viongozi makini hivyo siku ya Uchaguzi na wakati
huu lazima tuwapime wagombea wote kwasababu tunawajua vizuri,” alisema.
Kwa mujibu wa Dalali, baadhi ya wagombea hawana hadhi na uwezo wa
kuwa rais wa kwanza wa klabu hiyo, kutokana na fikra zao kuwa fupi.