Thursday, May 15, 2014

SAMATTA NA ULIMWENGU KUTUA DAR JUMAMOSI VS ZIMBABWE

RAIS wa shirikisho la soka nchini Tanzania, Jamal Malinzi imepigana kiume kuwasiliana na mwenyekiti na mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi  na taarifa njema juu ya mawasiliano hayo ni kwamba washambuliaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu watawasili jumamosi mchana kwa ajili ya mchezo wa jumapili.
SamataTaarifa za uhakika kutoka ndani ya TFF zinaeleza kuwa Rais Malinzi amethibitisha ujio wa wanandinga hao tegemeo kwa Taifa stars na kuibua matumaini ya Taifa stars kufanya vizuri kwasababu Samatta na Ulimwengu ni wachezaji mahiri zaidi kwa sasa.
Nyota hao wawili watatumiwa kwa mara ya kwanza na kocha wa Taifa stars, Mart Nooij katika mechi ya raundi ya awali kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam