Friday, June 27, 2014

RASMI" MAHAKAMA YAAMUA UCHAGUZI WA SIMBA SC KUFANYIKA JUNI 29

BAADA ya mvutano wa hapa na pale katika uchaguzi wa Simba sc sasa tamati imefika baada ya mahakamu kuu kuruhusu mchakato huo kuendelea kama kawaida.
Baadhi ya wanachama wa Simba walienda mahakama kuu wakihitaji chombo hicho cha dola kusimamisha uchaguzi wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwa
ka huu.
Sababu ya wanachama hao ilikuwa ni kupinga maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Damas Daniel Ndumbaro, kuliengua jina la aliyekuwa mgombe wa Urais, Michael Wambura kwa mara ya pili.
Hata hivyo, suala la wanachama kupelekea suala la michezo katika mahakama ya kawaida ilikuwa ni hatari zaidi kwa klabu ya Simba kwasababu sheria za mpira ziko wazi na hairuhusiwi kupeleka mambo ya mpira mahakama za dola.
FIFA wanataka masuala ya mpira yasuluhishwe katika mifumo yake ya haki na si vinginevyo.
Kupeleka mambo ya mpira mahakama za kawaida ilikuwa moja ya sababu iliyokuwa na nguvu kumuengua Wambura kwa mara ya kwanza.
http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/05/Wanachama-Simba1.jpgHata hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na katibu mkuu wa Simba, Kamwaga jioni ya leo imesema kamati ya Uchaguzi ya Simba SC imesema kuwa inapenda kuwaalika wanachama wote wa Simba katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliopangwa kufanyika Keshokutwa Jumapili, Juni 29 mwaka huu, katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kamwaga alifafanua kuwa katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea 27 wanatarajiwa kushiriki na Kamati ya Uchaguzi imeazimia kwamba suala la muda litazingatiwa sana safari hii kutokana na ukweli wa kuwepo kwa wagombea wengi.