
hivyo basi wameamua kuwaalika
wanachama wanahabari kuona maendeleo ya uwanja wa Bunju Jinsi unavyo endelea ambapo
sasa umefika hatua nzuri kilicho baki ni kuanza kuweka nyasi.
Yote kwa yote Azam fc kwa hapa tz ndio timu pekee
ndio klabu ya Tanzania yenye uwanja wake wa kisasa kwa ajili ya mazoezi, mechi
za ligi kuu na michuano yote inayosimamiwa na shirikisho la soka barani Afrika,
CAF.
Katika
historia ya soka la Tanzania, Azam fc haiwezi kunusa ukongwe wa klabu mbili za
Simba na Yanga.
Hizi ni
klabu zenye mafanikio ndani na nje ya uwanja. Ni klabu zenye mashabiki kila
kona ya nchi hii.
Lakini
licha ya kukaa miaka mingi katika soka la ushindani nchini Tanzania na michuano
ya Kimataifa, Yanga na Simba hazijawahi kumiliki viwanja vyake vya mazoezi na
mechi za ligi kuu.
Kwa miaka
mingi sasa viongozi wanaopita katika klabu hizo wanakuja na ndoto za kujenga
viwanja, lakini zinayeyuka kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kuendekeza siasa
kuliko vitendo.