
Uchaguzi
Mkuu Simba ulipangwa kufanyika Juni 29 na uamuzi huu wa TFF uliotangazwa Leo
kwenye Mkutano wake na Wanahabari unaitaka Simba kuunda Kamati ya Maadili
ifikapo Juni 30 na Kamati hiyo ndio itakayoshughulikia masuala yote ya Maadili
kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Uamuzi
huu wa TFF unaendelea kumweka Madarakani Mheshimiwa Ismail Aden Rage hadi hapo
Uchaguzi utakapofanyika baada ya Katiba yao kurekebishwa na kujumuisha Kamati
ya Maadili.
Uchaguzi
wa Simba umekumbwa na vuta nikuvute Klabuni hasa baada ya Mgombea Michael
Wambura kuenguliwa kugombea Urais na Kamati ya Uchaguzi ya Simba na yeye kukata
Rufaa TFF ambako Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake
Wakili Julius Lugaziya, ilimpitisha na kuamua aruhusiwe kugombea.
Hivi
karibuni, Yanga walipitisha uundwaji wa Kamati ya Maadili ya Klabu yao ili
kutii amri ya TFF kwenye Mkutano Mkuu wao huko Bwalo la Polisi –Oysterbay,
Jijini Dar es Salaam.
Lakini
hatua hiyo ililazimu Mkutano huo kumwongezea muda wa Mwaka mmoja Mwenyekiti wa
Klabu hiyo, Yusuf Manji, ili aweze kukamilisha masuala ya marekebisho ya Katiba
yao na kujumuisha Kamati ya Maadili na pia kuweza kuandaa Mkutano wa Uchaguzi
baada ya Katiba mpya kupitishwa na TFF.