
Malinzi ametoa kauli
hiyo katika futari aliyoandaa jana kwa wadau mbalimbali wa michezo
kikiwemo kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17,
Serengeti Boys katika ofisi za shirikisho hilo, Dar es Salaam. Malinzi
amesema ana uhakika kuwa balaa hilo la upangaji mechi za kimataifa
limeingia Afrika huku wanaofanya shughuli hizo wakiwashawishi viongozi,
makocha na hata wachezaji ili matokeo yapatikane wanavyotaka
wao.
Malinzi amesema sio suala la kuficha tena kuhusu janga hilo na
kuwaomba wadau na viongozi wa dini waliokuwepo katika shughuli hiyo
kuungana ili kuwakemea vijana wao kuhusu suala hilo. Mojawapo ya
viongozi mbalimbali waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es
Salaam Ramadhani Madabida, Katibu Mkuu wa zamani wa TFF enzi hizo
ikiitwa FAT Said El Maamry na viongozi mbalimbali wa timu za Ligi Kuu na
Ligi Daraja la kwanza Tanzania bara.