SIO NDOKI NG"O MAN CITY - TOURE NIPO SANA

KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City,
Yaya Toure amesema kuwa hana mpango wa kuondoka kwa mabingwa hao wa
Ligi Kuu na kudai ataendelea kuwepo hapo kwa msimu mwingine
unaokuja. Toure aliiambia luninga ya Sky Sport kuwa mashabiki wa timu
hiyo wamekuwa wema kwake na kwa familia hivyo ameona ni bora abaki kwa
ajili yao. kuhamia
katika vilabu mbalimbali toka wakala wake Dimitry Seluk Vyombo vya habari vimekuwa vikimhusisha kiungo huyoalipoandika
katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa nyota huyo
hajatulia. Seluk alitoa madai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory
Coast hakupewa utambulisho rasmi na klabu katika siku yake ya kuzaliwa
wakati wa safari yao ya Abu Dhabu huku Toure mwenyewe akiunga mkono
kauli hiyo. Toure amesema kwasasa mambo yote yako sawa na baada ya
tetesi nyingi kuzungumziwa juu yake anaaka kufanya kitu kwa ajili ya
mashabiki. Nyota huyo alijiunga na City akitokea Barcel
ona mwaka 2010 na
haraka alijitengenezea jina na kua mchezaji tegemeo wa timu hiyo
aliyoisaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2011 na mataji mawili ya Ligi
Kuu mwaka 2012 na 2014.