Mohamed Salah Mchezaji
wa Chelsea huenda asiichezee tena Chelsea kwa Kipindi cha
Miaka Mitatu baada ya kuitwa Nchini kwao ili aende Jeshini kwa Mujibu
wa Sheria.
Hivi sasa imeripotiwa kuwa Wizara ya Elimu ya Juu ya Misri imefuta
Masomo hayo na kumtaka arudi Misri mara moja ili atumikie Jeshini kwa
Mujibu wa Sheria kwa Kipindi cha kuanzia Mwaka Mmoja hadi Mitatu.
Hata hivyo, Mchambuzi wa Soka kutoka Misri alisema vitu hivyo ni
kawaida huko kwao na mara nyingi Mastaa wanaowakilisha vyema Nchi zao
huruhusiwa kuendelea na shughuli zao bila bughudha.
Hivi sasa, Chama cha Soka cha Misri, Makocha wa Timu ya Taifa ya
Misri na Maafisa wa Wizara ya Elimu ya Juu ya Misri, wameandaa Kikao ili
kuangalia nini cha kufanya kuhusu Salah.
Vile vile, Meneja wa Timu ya Taifa ya Misri, Shawky Gharib, amemwomba
Waziri wa Vijana kusaka suluhisho la tatizo hilo ili kumruhusuSalah
arejee Misri Mwezi Septemba kuichezea Nchi hiyo kwenye Mechi za Makundi
za kuwania Nafasi za kucheza Fainali za AFCON 2015 huko Morocco Mwakani.
Ikiwa hali ya sasa itaendelea Salah akirudi kwao tu hataruhusiwa
kutoka nje ya Nchi hadi atumikie Jeshi kwa Kipindi hicho cha Mwaka mmoja
hadi mitatu.
Personal information | |||
---|---|---|---|
Full name | Mohamed Salah Ghaly | ||
Date of birth | 15 June 1992 | ||
Place of birth | Basion, El Gharbia, Egypt | ||
Height | 1.75 m (5 ft 9 in) | ||
Playing position | Winger | ||
Timu ya sasa | |||
Current team
|
Chelsea | ||
Number | 15 | ||
Timu za vijana | |||
2006–2010 | El Mokawloon | ||
Timu za ukubwani | |||
Years | Team | Mechi | (Goli) |
2010–2012 | El Mokawloon | 41 | (11) |
2012–2014 | Basel | 47 | (9) |
2014– | Chelsea | 10 | (2) |
Timu ya taifa | |||
2010–2011 | Egypt U20 | 11 | (3) |
2011–2012 | Egypt U23 | 11 | (4) |
2011– | Egypt | 29 | (17) |