Friday, July 18, 2014

UEFA YAWEKA HADHARANI MAJINA 10 KUWANIA MCHEZAJI BORA ULAYA!

Katika kuelekea katika michuano ya Uefa champions Ligi Jana UEFA imetoa Majina ya wanandinga 10 Wanao gombea Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka na Mshindi atatangazwa hapo Agosti 28 wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na hao 10 ndio kuibuka kidedea.
Lakini Majina hayo 10 yatachujwa kwa Kura hapo Agosti 14 na kubakisha Majina Matatu yatakayopigiwa Kura na kutangazwa Mshindi hapo Agosti 28.
WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Miongoni mwa Majina makubwa ambayo hayamo kwenye Listi hii ya Wachezaji 10 ni yale ya Zlatan Ibrahimovic, Gareth Bale na Neymar.
JAMES-RODRIGUEZ-COLOMBIALakini yapo Majina ya Wachezaji Watatu toka Kikosi kilichochukua Kombe la Dunia cha Germany Jumapili iliyopita huko Brazil na pia yupo James Rodriguez alietwaa Buti ya Dhahabu huko Brazil kwa kuwa Mfungaji Bora wa Kombe la Dunia akiichezea Nchi yake Colombia.
Bila kustajabisha, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa Wagombea.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Klabu.
LISTI YA WAGOMBEA 10:
-Diego Costa [Spain, Atletico Madrid]
-Angel Di Maria [Argentna, Real Madrid]
-James Rodriguez [Colombia, AS Monaco]
-Luis Suarez [Liverpool (Sasa Barcelona), Uruguay]
-Philipp Lahm [Germany, Bayern Munich]
-Thomas Muller [Germany, Bayern Munich]
-Manuel Neuer [Germany, Bayern, Munich]
-Arjen Robben [Germany, Bayern Munich]
-Cristiano Ronaldo [Portugal, Real Madrid]
-Lionel Messi [Argentina, Barcelona]