MABINGWA wa Tanzania VPL,
Azam fc wametolewa nje katika michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika
Mashariki na kati, Kombe la Kagame kwa kufungwa penalty 4-3 dhidi ya El
Merreik ya Sudan katika mchezo wa robo fainali.
Mshindi wa mchezo huo uliopigwa katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda, alilazimika kupatikana kwa changamoto ya matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana (0-0)