Simba ya Patrick Phiri iko kambini Unguja na Yanga ya Marcio Maximo jana Jumatatu imetua Pemba. Msolla amesema Azam imejiweka kwenye nafasi nzuri timu anazocheza nazo huko Rwanda ni za kiwango cha kimataifa timu hizo zitaweza kuwapima vizuri na kuwasaidia pia wakirejea watakuwa na muda wa kama wiki tatu kurekebisha makosa yao.
Simba na Yanga wao nimesikia wameweka kambi Zanzibar napata wasiwasi kama wataweza kupata mechi kubwa za kirafiki kutokana na muda kwenda wasijidanganye kucheza na timu za Zanzibar kwani timu za kule ziko chini, ligi yao si ya ushindani kama ya Bara.Wakishindwa kuwa na mechi kubwa za kirafiki watapata shinda mwanzo wa msimu kwani watakuwa hawajakomaa vizuri, pia katika mechi hizo lazima wazingatie ngazi waliyopo, kwa mfano Simba ilicheza na Zesco wakati ikiwa kwenye ngazi za awali, ile haikuwa kipimo tosha.