Tuesday, August 19, 2014

POLISI MORO WAJIGAMBA KUHUSU MRWANDA NA MACHAKU

POLISI Morogoro imeweka wazi kombinesheni ya washambuliaji wao wapya, Danny Mrwanda, Salum Machaku na Six Mwasekaga iko vizuri na wanachokifanya sasa ni kuwatengenezea mfumo wa kisasa utakaowaunganisha na viungo pamoja na mabeki wawatengenezee nafasi nyingi za mabao.
Benchi la ufundi la kikosi hicho chini ya kocha mkuu,Adolf Rishard na msaidizi wake, John Tamba wanawatengeneza mfumo ambao utawafanya mabeki na viungo kuwatengenezea washambuliaji hao nafasi nyingi za mabao.
Tamba amesema Kombinesheni ya Machaku, Mrwanda na Mwasekaga iko vizuri na ili kuwaongezea ubora, tunatengeneza mfumo mzuri wa kisasa utakaokuwa na muunganiko kunzia beki, kiungo ambao watawapa nafasi nzuri za kufunga washambuliaji.”