Tuesday, August 26, 2014

MAXIMO ASEMA ANAWATAMBUA WACHEZAJI WATANO TU YANGA.

Kocha mkuu Mbrazil kwenye Ligi ya Tanzania, Marcio Maximo ametamka kuwa anawajua wachezaji watano tu wa kigeni Yanga na ndio atakaowatumia Miongoni mwao jina la Okwi ambaye yupo Dar es Salaam halimo.
Maximo amesema atafanya kazi na Hamis Kiiza raia wa Uganda, Wanyarwanda Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite pamoja Wabrazili Andrey Coutinho na Genilson Santos ‘Jaja’ ndiyo anaowatambua.
Pamoja na wachezaji hao watano wanaofanya mazoezi ya pamoja, Yanga ina mkataba na Okwi anayefanya timu kuwa na wachezaji sita wa kigeni idadi ambayo hadi kesho Jumatano siku ya kufunga dirisha la usajili lazima ipunguzwe kwa mmoja kutupiwa virago.
Maximo amesema Okwi sijamwona na hajaripoti kwenye timu yangu nifanyaje". Nitafanya kazi na hao tu ambapo awali Kiiza ndiyo alikuwa aachwe, lakini sasa hali imeanza kuwa shwari kwake kutokana na nidhamu yake na jinsi anavyojituma mazoezini.
Okwi ambaye alikuwa anapewa kipaumbele lakini alichelewa kujiunga na timu kwa sababu zisizojulikana, inadaiwa kuwa uongozi umemwambia ajieleze kwa barua na baada ya hapo atapewa adhabu ambayo ni siri.Okwi alichelewa kuja kambini kujiunga na Yanga kwa madai kwamba hajalipwa fedha zake.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva ambaye pia ni Mbrazili amesema wamefurahishwa na uwezo wa  Kiiza na kukiri kuwa ana sababu zote za kubaki Yanga.