Saturday, November 22, 2014

HENRY ATARAJIWA KUTUA KWA WENGER KUWA MKUFUNZI.

Timu ya Arsenal ipo katika harakati za kumpatia aliyekuwa mshambulizi wa timu hiyo Thiery Henry fursa ya ukufunzi katika timu hiyo kulingana na gazeti la daily mail.
Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa katika kilabu ya New York Red Bulls inatarajiwa kuisha mwisho wa msimu wa ligi ya soka ya marekani MLS mwezi ujao na hajasema ni hatua gani anayotarajia kuchukua.
Wengi wanaamini kwamba kampeni hiyo itakamilisha harakati zake kama mchezaji na huenda Arsene Wenger akamchukua katika klabu hiyo.
Na alipoulizwa iwapo Henry anaweza kurudi katika klabu hiyo kama kocha ,Wenger alijibu kwamba hakuna lisilowezekana.''Mimi huwakaribisha watu ambao wameichezea timu hii''.
Nimewaona wengi ambao wana uwezo lakini wameshindwa katika fursa yao ya kwanza kwa kuwa hawakuwa tayari.