Simba imeamua kufanya mabadiliko tena katika benchi la ufundi na nguvu zimeelekezwa kwa Kocha Mdenishi, Kim Poulsen.
Poulsen raia wa Denmark katika nafasi ya Mzambia Patrick Phiri ambaye timu yake imecheza mechi sita mfululizo na kutoka sare zote.Simba imeingia kwenye harakati za kumng’oa Phiri ambaye ameingoza Simba katika mechi sita tu za Ligi Kuu Bara na zote ametoka sare. Simba imefunga mabao sita, imefungwa sita na ina pointi sita.
Mdenishi Poulsen ambaye yuko kwao nchini Denmark baada ya kuzinoa timu za taifa za vijana na baadaye Taifa Stars, aliondolewa kwenye kiti chake baada ya kuingia kwa uongozi wa Jama Malinzi.Habari za uhakika kimesema kuwa Simba wamefanya mazungumzo na Poulsen na kukubaliana kila kitu na yuko tayari kucha nchini wakati wowote.

Hivyo wanachosubiri huenda kikawa ni mechi ya Jumamosi na kama si mechi hiyo, basi angekuwa ameishatua,” kilifafanua chanzo.
Iwapo Simba itashikilia msimamo wake wa kumleta Poulsen, basi lazima itaendelea na rekodi yake ya kuwa tim iliyofukuza makocha wengi zaidi kwa misimu mitatu mfululizo.
Katika misimu miwili iliyopita, Simba ilifundishwa na makocha wanne tofauti, kila mmoja akifundisha nusu msimu ambao ni Abdallah Kibadeni Mputa,Patric liewing,Logarusic na huyu Patric Phiri
Source: Champion