
Golikipa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anaungana na Cesc Fabregas anayetumikia adhabu kuwa wachezaji ambao wataukosa mchezo huo wakati Chelsea wakijaribu kurejesha makali yao baada ya kipigo kutoka kwa Newcastle United mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mourinho aliendelea kudai kuwa Fabregas amekuwa na msaada mkubwa katika kikosi chake lakini hawatakuwa naye katika mchezo wa kesho akitumikia adhabu yake ila wana wachezaji wengine anaowaamini.
Mourinho sasa atalazimika kuendelea kumtumia Petr Cech ambaye alimtumia pia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon Jumatano iliyopita.