
Marekani imebainisha kuwa
mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za
Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi
ya wahusika wa kashfa hiyo.
Haya yanajiri wakati Rais
Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge
kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti
ya Tegeta Escrow wiki ijayo.
Katika tamko hilo kwa umma
ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa
kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya
Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi
dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL.
Taarifa iliyotolewa na
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC
waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa
na hali ya rushwa nchini Tanzania.
Uamuzi huo wa Marekani
ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa
Rais Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo
mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.

Wengine ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Jaji Frederick Werema.
Novemba mwaka huu, Serikali
ya Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku ya hadi Dola za Kimarekani
milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya uwekezaji yenye matokeo
makubwa katika sekta ya nishati nchini.
Tanzania ilikuwa mojawapo ya
nchi kumi zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo
zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.

Juhudi za BBC kumtafuta
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress,aweze kuzungumzia juu ya
ripoti hiyo ziligonga mwamba kutokana na sababu za kiprotokali .