MENEJA
wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amehatarisha kuwaudhi zaidi mashabiki wa
timu hiyo baada ya kudai kuwa hatakuwa na haja ya kufanya usajili katika
kipindi cha dirisha dogo Januari mwakani kama wachezaji wote katika kikosi
chake cha sasa watakuwa fiti.

Wenger
alishambuliwa na mashabiki wenye hasira katika kituo cha treni wakati akirejea
London baada ya mchezo dhidi ya Stoke.
Pamoja
na kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa alama 13 Wenger bado bado anaonesha
kutoshtushwa na hali hiyo kwa kudai kuwa hatarajii usajili wa Januari kuwa
pilikapilika kubwa.
Wenger
amesema kama wachezaji watakuwa fiti na uwezo wa kucheza hadhani kama atahitaji
kufanya usajili wa aina yeyote.