BEKI
wa Real Madrid, Raphael Varane amabainisha kuwa ilibaki kidogo ajiunge na
Manchester United kabla ya kukamilisha usajili wake Santiago Bernabeu.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Ufaransa, alijiunga na Madrid akitokea klabu ya Lens mwaka
2011 kwa kitita cha euro milioni 10.
Hata
hivyo, Varane amekiri kuwa alikuwa akifikiria kwenda Old Trafford lakini
akaamua kwenda Maddrid kwani aliona ndio mahali pazuri kwa kuimarika kama
mchezaji.
Varane
amesema walikuwa wamekaribia kukubaliana na United kwnai mama yake anazungumza
lugha ya kiingereza hivyo ndio alikuwa kama mkalimani lakini baada ya kufikiri
sana akaona bora aende Madrid.