Tuesday, December 16, 2014

UONGOZI WA CLUB YANGA WASAMBARATISHA BENCHI LAKE LA UFUNDI

Uongozi wa club ya Yanga umewatupia virago Wabrazil, Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Leiva na kuwarejesha Mholanzi, Hans van der Pluijm na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa.
Maximo ametupiwa virago na baada ya kipindo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe.
Pluijm atamewasili  jana 8:38 usiku na kuweka kandarasi ya Mkataba wa kuanza kazi ambapo Mkwasa tayari alisaini Mkataba wiki kadhaa zilizopita na ameridhika kufanya kazi chini ya Pluijm tena.
Maximo na Leonardo walitua Yanga SC Julai mwaka huu kurithi mikoba ya Pluijm na Mkwasa ambao walipata kazi Uarabuni.
Hata hivyo baada ya muda usiozidi mwezi mmoja, Pluijm na Mkwasa waliacha kazi Uarabuni, wakidai kukerwa na kuingiliwa na viongozi wa klabu yao katika masuala ya kiufundi.
Pluijm alirudi Ghana wakati Mkwasa alirejea nyumbani Tanzania kabla ya kuajiriwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Mkufunzi Mkuu.
Hadi anaondoka Yanga SC, Maximo ameiongoza timu hiyo katika mechi 14, kati ya hizo akishinda 10, sare moja na kufungwa tatu dhidi ya Kagera Sugar 1-0, Mtibwa Sugar 2-0 sawa na Simba SC katika Mtani Jembe. 
Pluijm aliiongoza Yanga SC katika mechi 19, akishinda 11, sare sita na kufungwa mbili dhidi ya Al Ahly 1-0 Cairo na Mgambo JKT 2-1 Tanga.
Yanga SC ilikuwa tayari kuendelea na Maximo iwapo angekubali kufanya kazi na Mkwasa, lakini baada ya kukataa, klabu imeoana bora kuachana naye.
Maximo alikuwa anafanya kazi kwa mara ya pili Tanzania, baada ya awali kuwa kocha wa timu ya soka ya taia, Taifa Stars kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.
REKODI YA PLUIJM AIKIWA NA YANGA SC
Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki)
Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki)
Yanga SC 2-1 Ashanti United (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
Yanga SC 5-2 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
Yanga SC 7-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu ya Bara)
Yanga SC 1-0 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa)
Yanga SC 0-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa.
Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)
Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar  (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
Yanga SC 5-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)

Yanga SC 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)