
Mbali ya kuwahi kuwa mchezaji
katika timu ya RTC Kagera, Kocha Madega aliwahi kufundisha timu za Kagera
Stars, Mwadui na kombaini ya Copa Coca-Cola ya Mkoa wa Kagera.
Mchango
wake katika mchezo wa mpira wa miguu tangu akiwa kocha na baadaye kocha
utakumbukwa daima.
Tunatoa salama za rambirambi kwa
familia ya marehemu, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Chama cha
Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa Kagera na klabu ya Bukoba
Veterans na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo.
TFF
itawakilishwa kwenye msiba huo na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera
(KRFA).