Tuesday, December 16, 2014

YANGA WAKALI KWELI KWELI YAMTUPIA VIRAGO EMERSON NA KIIZA

Baada ya Mvutano wa hapa na pale nani aachwe kati ya Emerson kiiza na Coutinho Yanga sasa imeamua kuwaacha kuwatupia virago Mbrazil, Emerson de Oliviera Roque na Mganda Hamis Kiiza na kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mrundi Amisi Tambwe.
Tambwe amesaini Mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachwa na klabu yake, Simba SC aliyoichezea msimu mmoja uliopita akitokea Vital’O ya Burundi.
Yanga SC imeamua kumuacha Mbrazil Emerson baada ya kushindwa kupata Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Tambwe anaungana na Mliberia, Kpah Sherman, Wanyarwanda Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Mbrazil Andrey Coutinho kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni Yanga SC.
Wakati dirisha la usajili limefungwa jana Saa 6:00 usiku.
Yanga SC imesajili jumla ya wachezaji watatu wapya baada ya kumuacha Emerson, mwingine ni Danny Mrwanda. 
Katika kipindi cha msimu mmoja, Tambwe ameichezea Simba SC jumla ya mechi 43 na kuifungia mabao 26.
Maisha yake yalianza kuwa magumu Simba SC baada ya ujio wa kocha Mzambia, Patrick Phiri kuchukua mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic.