Usajili
wa dirisho dogo msimu wa 2014/2015 umefungwa jana (Desemba 15 mwaka huu) huku
wachezaji 15 kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka
nchi mbalimbali.
Wachezaji
walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya
Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam,
Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles
Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael
Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Dan
Serunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves
Roque kutoka Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil)
kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na
Juuko Murushid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.
Kpah Sean
Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya)
kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand
United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge
Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Serunkuma kutoka
Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili
wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo.