SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza orodha ya wachezaji watatu watakaogombea tuzo ya mchezaji ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia maarufu kama Ballon d’Or.

Sherehe za utoaji tuzo inatarajiwa kufanyika Januari 12 mwakani huku Ronaldo akiwa ndio mshindi wa mwaka jana. Kwa upande wa wanawake walioteuliwa kugombea tuzo hiyo ni pamoja na Nadine Kessler wa Ujerumani, Marta wa Brazil na Abby Wambach kutoka Marekani.
Kwa upande wa makocha walioteuliwa kugombea tuzo ni pamoja na Carlo Ancelotti wa Real Madrid, Joachim Loew aliyeiwezesha Ujerumani kunyakuwa Kombe la Dunia na kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone.