Tuesday, April 23, 2013

KOCHA KIM ATANGAZA YOUNG TAIFA STARS
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.

Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.

“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.

Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta (Simba).

Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).

AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon na JKT Ruvu.

Mechi hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari Kambangwa, Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
VAN MAGOLI JEZI 20 APIGA TATU NA KUILETEA UBINGWA WA 20 MAN U:
Katika mechi ya jana Robin van Persie, amefanya kile ambacho wadau na mashabiki wa man u ambao waliondoa imani naye kuwa haufumanii nyavu lakini aliweza kudhihilisha kuwa yeye ni bora zaidi baada ya kutupia Bao Dakika za 2, 13 na 33 na, kufuatia kazi nzuri ya Nguli Ryan Giggs na Wayne Rooney, na kuwatwanga Aston Villa Bao 3-0 Uwanjani Old Trafford na kuipatia Manchester United Ubingwa wa BPL, Barclays Premier League huku wakiwa na Mechi 4 mkononi.
HISTORIA:
.Hii ni mara ya 4 kwa Man United kutwaa Ubingwa Uwanjani kwao Old Trafford
.Mara nyingine walizotwaa Ubingwa Old Trafford ni Mwaka 1999, 2002 na 2009
.Mwaka 2001 walitwaa Ubingwa wakiwa na Mechi 5 mkononi
.Msimu wa 1999/2000 walitwaa Ubingwa kwa pengo la Pointi 18
kwa sasa Van Persie  anaongoza Ufungaji Bora BPL akiwa na Bao 24 kwa mtukutu Luis suarez akiwa na mabao 23.
Huu ni Ubngwa wa 13, chini ya Sir Alex Ferguson, katika Miaka 21 ya Historia ya Ligi Kuu England.
MSIMAMO==BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
34
40
84
2
Man City
33
29
68
3
Arsenal
34
30
63
4
Chelsea
33
31
62
5
Tottenham
33
17
61
6
Everton
34
13
56
7
Liverpool
34
19
51
8
West Brom
33
-1
45
9
Swansea
33
1
42
10
West Ham
34
-7
42
11
Fulham
34
-8
40
12
Southampton
34
-7
39
13
Norwich
34
-20
38
14
Sunderland
34
-7
37
15
Stoke
34
-11
37
16
Newcastle
34
-17
37
17
Aston Villa
34
-27
34
18
Wigan
33
-23
31
19
QPR
34
-27
24
20
Reading
34
-28

24

PFA KUMPA USHAURI MZEE WA MENO
CHAMA cha Wanasoka wa Kulipwa-PFA kimesema kuwa mshambuliaji nyota wa Liverpool, Luis Suarez atapatiwa ushauri wa namna ya kuzikabili hasira zake kufuatia tukio lake la kumg’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay tayari ameshamuomba radhi Ivanovic kwa tukio hilo alilofanya katika mchezo wa ligi baina ya timu hizo ambao uliisha kwa sare ya mabao 2-2 lakini klabu yake imeshamtoza faini na kunauwezekano mkubwa FA nao wakatoa adhabu baadae. Suarez mwenye umri wa miaka 26 alifungiwa kucheza mechi saba baada ya kufanya tukio kama hilo wakati akiwa katika klabu ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi kipindi cha nyuma ambapo alimng’ata Otman Bakkal wa PSV. Nyota huyo asiyetabirika pia alishawahi kufungiwa mechi nane katika Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United. Ofisa Mkuu wa PFA Gordon Taylor amesema hakuna shaka juu ya kiwango bora alichonacho nyota huyo lakini inasikitisha kwa vitendo vya ambavyo amekuwa akivifanya ndio maana wameamua kumsaidia ili aweze kuzikabili hasira zake.


Monday, April 22, 2013

FA USO KWA USO SUAREZ HUKU CLUB YAKE PIA IKIMTWANGA FAINI

 Chama cha Soka cha England "FA" kimetangaza kumfungulia Mashitaka Straika wa Liverpool Luis Suarez, kwa Kosa la kuleta vurugu Uwanjani kwa kumng’ata meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.


Tukio hilo lilitokea Uwanjani Anfield Liverpool ilipotoka sare ya 2-2 na Chelsea katika Mechi ya BPL, Barclays Premier League lakini Refa Kevin Friend hakuliona kama ilivyothibitishwa na FA kufuatia Ripoti ya Refa na hivyo wao kupata fursa kumfungulia mashitaka kwa kutumia ushahidi wa Mikanda ya Video.
Mara baada ya tukio hapo Uwanjani Ivanovic alionekana akimuonyesha Refa Friend alama za meno mkononi mwake.
SUAREZ_KIDOLEFA pia imetamka kuwa kawaida makosa kama hayo ni Kifungo cha Mechi 3 lakini kwa tukio hilo Adhabu hiyo haitoshi.
Suarez amepewa had Aprili 23 Saa 2 Usiku mwaka huu awe amejibu Mashitaka hayo na
 Jumatano Aprili 24, Jopo Huru la FA litaketi kusikiliza Kesi hiyo.
Tayari Suarez ameshaomba radhi kwa kumuuma meno Ivanovic na kuongea na Beki huyo wa Chelsea.
Liverpool pia imetangaza kumpiga Faini lakini imesisitiza ataendelea kubakia kuwa Mchezaji wao.

OLIVIER GIROUD: ARSENAL KUPAMBANA KADI NYEKUNDU

Washika bunduki wa jiji la london  Arsenal chini ya meneja wenger" wamewasilisha Rufaa yao kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Straika wao mahili  Olivier Giroud Juzi Jumamosi Arsenal walipoifunga Fulham Bao 1-0 Uwanjani Craven Cottage kwenye Mechi ya Ligi.
Giroud alitolewa kwa kumchezea Rafu Stanislav Manolev.
Akielezea tukio hilo baada ya Mechi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema: “Giroud aliniambia aliteleza wakati akifuata Mpira na hilo limethibitishwa na Mikanda ya Video.”
Jopo Huru la FA litatoa uamuzi wake Siku ya Jumanne.
Ushindi huo wa Arsenal dhidi ya Fulham ulikuwa ushindi wao wa 5 katika Mechi 6 za Ligi na umezidi kuwaimarisha katika azma yao ya kumaliza kwenye 4 Bora.
Arsenal sasa wapo nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 63.
Tangu ajiunge na Arsenal kutoka Montpellier mapema mwanzoni mwa Msimu huu, Giroud amepachika Bao 17 katika Mechi zake 46 na Arsenal.
ARUDI TENA NDANI YA STAMFORD BRIDGE"
CLATTENBURG1
REFA Mark Clattenburg anatajiwa kurudi katika dimba la Stamford Bridge kuichezesha Chelsea kwa mara ya kwanza tangu asafishwe suala la Ubaguzi dhidi ya John Obi Mikel na huko Emirates, Arsenal i
CLATTENBURG NA CHELSEA
JUMAPILI, Refa Mark Clattenburg atarudi Uwanja wa Stamford Bridgekuichezesha Chelsea kwa mara ya kwanza baada ya Miezi 6 baada ya kusafishwa kutumia Ubaguzi dhidi ya Kiungo wa Chelsea John Obi Mikel.
Chelsea walilalamika kuwa Clattenburg alitumia lugha isiyofaa dhidi ya Mikel wakati wanachapwa Bao 3-2 na Manchester United Mwezi Oktoba Mwaka jana Uwanjani Stamford Bridge.
Baada ya uchunguzi wa FA, Refa huyo, ambae alitamka jambo hilo limemtisha, Clattenburg alisafishwa kuhusu tuhuma zote.
Baadae Klabu ya Chelsea ilitoa tamko la kusikitika kuhusu walivyochukulia suala hilo na kutaka radhi na sasa, Miezi 6 baadae, Clattenburg ataichezesha Chelsea watakapocheza na Swansea City 

RAIS TENGA ATOA MIPIRA YA DOLA 30,000

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa mipira zaidi ya 1,200 yenye thamani ya dola 30,000 za Marekani kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na vituo 21 vilivyo hai vya kuendeleza vijana (academies).

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) lilimpa Rais Tenga fedha hizo ikiwa ni shukrani kwake kwa kushughulikia mgogoro wa uongozi wa mpira wa miguu nchini Kenya uliodumu kwa miaka miwili; ambapo nchi hiyo kutokana na mgogoro huo ilikuwa na vyama viwili (KFF na FKL).

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mipira hiyo kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam leo (Aprili 22 mwaka huu), Rais Tenga amesema amefanya hivyo kwa vile anaamini kuwa mipira ndiyo kitu muhimu katika kuinua mchezo huo mahali popote.

“Dhamira yangi si kushukuru kwa hafla hii, bali kutoa sababu kwa nini nimefanya hivi. Ninaamini kwa kuanzia mipira ndiyo muhimu, pili kwa kufanya hivi itaonekana kweli mipira imegawiwa,” amesema Rais Tenga.

Amesema amesema mpira wa miguu kwa Tanzania unahitaji sana watu wa kujitolea, na yeye amefanya hivyo kwa kujitolea kutokana na ukweli shughuli anazotumwa na FIFA ni za kujitolea.

Rais Tenga ambaye pia alitumwa na FIFA kutatua matatizo ya uongozi wa mpira wa miguu katika nchi za Uganda, Zambia na Sudan Kusini amesema anaamini anapata fursa hizo kutokana na kuwa kiongozi wa TFF, na kwa kuwakumbuka waliomchagua ndiyo maana hakusita kupeleka fedha hizo kwenye mipira.

Amesema moja ya ndoto zake wakati anaingia kuongoza TFF mwaka 2004 ameshindwa kutimiza ni kusaidia mipira, kwani uwezo wa kununua mipira kwa wanaocheza katika ngazi ya chini hasa watoto haupo.
“Hizi kelele zote za maendeleo ya mpira wa miguu ni kwa sababu shuleni hakuna vifaa. Nia yangu ilikuwa shule zote zipate mipira, lakini hiyo ni moja ya ndoto nilizoshindwa kutekeleza. Vipaji haziwezi kupatikana kama watoto hawachezi.

“Tunashukuru sana kwa Serikali kurejesha mpira shuleni. Hata nitakapoondoka madarakani nikipata nafasi nitaendelea kuomba mipira kwa ajili ya shule,” amesema Rais Tenga.

Vyama vya mikoa ambavyo jumla ni 32 (Tanzania Bara na Zanzibar) kila kimoja kimekabidhiwa mipira 25 (kumi saizi namba tano, 15 saizi namba nne kwa ajili ya vijana). Kwa academies ambazo ni 21 kila moja imepewa mipira 25 (minane saizi namba tano, na 15 saizi namba nne).

Viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Almasi Kasongo, Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) Nassib Mabrouk na Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) Riziki Majala.

Kwa upande wa shule alikuwa Kanali mstaafu Idd Kipingu ambaye ni mmiliki wa shule ya Lord Baden ya Bagamoyo mkoani Pwani.

COASTAL, AZAM KUCHEZA SIKU YA MUUNGANO
Timu za Coastal Union ya Tanga na Azam zitapambana Aprili 26 mwaka huu katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) itakayofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Awali mechi hiyo namba 168 ilikuwa ichezwe Aprili 27 mwaka huu, lakini imerudishwa nyuma kwa siku moja ili kuipa fursa Azam kujiandaa kwa mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco.

Mechi hiyo itachezeshwa na Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani akisaidiwa na Abdallah Mkomwa (Pwani), Vicent Mlabu (Morogoro) wakati mwamuzi wa mezani atakuwa Mohamed Mkono wa Tanga. Charles Komba wa Dodoma ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo ya raundi ya 24.

Baada ya mechi ya Tanga, Azam itarejea Dar es Salaam siku inayofuata tayari kwa safari ya kwenda Rabat itakayofanyika Aprili 28 mwaka huu. Mechi hiyo itachezwa wikiendi ya Mei 3, 4 au 5 mwaka huu.

Keshokutwa (Aprili 24 mwaka huu) kutakuwa na mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Iwapo Azam itafanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kutakuwa na marekebisho ya ratiba ya VPL. Hiyo ni kutokana na raundi inayofuata ya Kombe la Shrikisho kuchezwa wikiendi ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu ambapo bado haijajulikana Azam itaanzia wapi (nyumbani au ugenini) iwapo itavuka.

Mechi nyingine za VPL mwezi ni Aprili 25 (Ruvu Shooting vs Simba- Uwanja wa Taifa), na Aprili 28 (Simba vs Polisi Morogoro- Uwanja wa Taifa).

MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Kocha Mkuu wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Aprili 23 mwaka huu).

Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

WAMOROCCO WA AZAM WAINGIZA MIL 50/-
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na AS FAR Rabat ya Morocco iliyochezwa juzi (Aprili 20 mwaka huu) imeingiza sh. 50,850,000.

Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 8,268 waliokata tiketi.

Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 7,354.

Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 6,791,175, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 4,527,450 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 33,955,875.

Mechi iliyopita ya Azam katika michuano hiyo dhidi  ya Barrack Young Controllers II ya Liberia iliingiza sh. 44,229,000 kutokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi. Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A.

MECHI YA JKT RUVU, YANGA YAINGIZA MIL 66/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Yanga iliyochezwa jana (Aprili 21 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,568,000 kutokana na watazamaji 11,864.

Viingilio katika mechi hiyo namba 106 iliyomalizika kwa Yanga kutoa dozi ya 3-0 kwa wenyeji wao vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,702,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,154,440.68.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,984,450.40, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,790,670.24, Kamati ya Ligi sh. 4,790,670.24, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,395,335.12, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 931,519.21 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 931,519.21.
 Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
DROGBA VS ETOO KUWANIA TUZO GUU LA DHAHABU
WASHAMBULIAJI bora  barani Afrika, Didier Drogba na Samuel Eto’o
wameingizwa kwenye orodha ya kuwania tuzo ya Guu la Dhahabu mwaka 2013, kufuata nyayo za mshambuliaji wa Paris Saint Germain ya Ufaransa, Zlatan Ibrahimovic, aliyeshinda mwaka jana.
Manahodha hao wa Ivory Coast na Cameroon ni Waafrika pekee katika orodha ya wachezaji tisa walioingizwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzi hiyo, inayotolewa kwa wachezaji wenye mafanikio makubwa na mwonekano mzuri.
Wawania tuzo hiyo wengine ni Mfaransa David Trezeguet, Mjerumani Miroslav Klose, Mtaliano Andrea Pirlo, Waspanyola Andres Iniesta na Iker Casillas na Waingereza Franck Lampard na David Beckham.
Tuzo huyo Guu la Dhahabu inatolewa kwa mchezaji aliye uwanjani ambaye angalau ana umri usiopungua miaka 29 na hawezi kushinda zaidi ya mara moja
Washindi wa awali wa tuzo hiyo ni; 2003: Roberto Baggio (Italia, Brescia) 2004: Pavel Nedved (Jamhuri ya Czech, Juventus) 2005: Andryi Shevchenko (Ukraine, AC Milan) 2006: Ronaldo (Brazil, Real Madrid) 2007: Alessandro Del Piero (Italia, Juventus) 2008: Roberto Carlos da Silva (Brazil, Fenerbahçe) 2009: Ronaldinho (Brazil, AC Milan) 2010: Francesco Totti (Italia, Roma) 2011: Ryan Giggs (Wales, Manchester United) na 2012: Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris SG).

TAZAMA MECHI WALIZO CHEZA NA MAGOLI WALIOFUNGA
 Didier Drogba Games/Goals
2009/10 Chelsea 21/17
2008/09 Chelsea 24/5
2007/08 Chelsea 19/8
2006/07 Chelsea 36/20
2005/06 Chelsea 29/12
2004/05 Chelsea 26/10
2003/04 Marseille 35/19
2002/03 Guingamp 34/17
2001/02 Guingamp 10/3
2001/02 Le Mans 21/5
2000/01 Le Mans 11/0
1999/00 Le Mans 30/7
1998/99 Le Mans 2/0
TOTAL: 298/123

Samuel Eto
'o Games/Goals
2009/10 Inter 19/8
2008/09 Barcelona 36/30
2007/08 Barcelona 18/16
2006/07 Barcelona 17/11
2005/06 Barcelona 34/27
2004/05 Barcelona 37/25
2003/04 Mallorca 32/17
2002/03 Mallorca 29/14
2001/02 Mallorca 29/6
2000/01 Mallorca 25/11
1999/00 Mallorca 9/6
1999/00 R Madrid 2/0
1998/99 R Madrid 1/0
1997/98 Leganes 28/3
TOTAL: 316/174
  

BONDIA wa uzito wa juu wa Uingereza, Dereck Chisora amefanikiwa kumchakaza Hector Alfredo Avila katika raundi ya tisa likiwa ni pambano lake la kwanza toka alipopata kipigo kutoka kwa David Haye Julai mwaka jana. Chisora mwenye umri wa miaka 29 alikuwa akipigana pambano lake la kwanza toka aliporejeshewa leseni yake Machi mwaka huu baada ya leseni hiyo kuzuiwa kufuatia vurugu za nje ya ulingo alizofanya na Haye mapema mwaka huu. Akihojiwa mara baada ya kumpiga Avila ambaye ni raia wa Argentina Chisora amesema lilikuwa pambano gumu kwasababu mpinzani wake alikuwa amempania lakini anashukuru amemaliza kwa ushindi na anasubiri mpinzani mwingine. Chisora anasubiri pambano linguine dhidi ya bondia mwingine wa uzito wa juu wa Uingereza David Price ambaye kabla ya kupambana na Chisora atapigana na Tony Thompson katika pambano la marudiano Julai mwaka huu.

NUSU FAINALI UEFA CHAMPION LIGI KESHO WANAUME DIMBANI
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu]
Jumanne Aprili 23
Bayern Munich v Barcelona
Jumatano Aprili 24
Borussia Dortmund v Real Madrid
MARUDIANO
Jumanne Aprili 30
Real Madrid v Borussia Dortmund
Jumatano Mei 1
Barcelona v Bayern Munich
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, Londo
SUAREZ BADO AENDELEZA VITUKO KATIKA SOKA WADAU WAMSHANGAA
BOSI wa Liverpool, Brendan Rodgers, amekiri kutoona tukio la Straika wake mahili Luis Suarez  wakati akimng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic bila Refa Kevin Friend kuona, FA imesema itapitia Mkanda huo na Ripoti ya Refa ili kutoa mwelekeo huku Wachambuzi wa Soka huko England wakilaani vikali kitendo hicho.
Brendan Rodgers ameahidi kupitia Mkanda wa Video wa tukio hilo na kutoa tamko lakini Meneja wa zamani wa Liverpool, Graeme Souness, amelaani vikali tukio hilo na kusema umefika wakati wa Mchezaji huyo kutoka Uruguay kuondolewa Liverpool.
Souness ameng’ang’ania kuwa Liverpool ni Klabu kubwa yenye hadhi kama Barcelona, Real Madrid a Manchester United, na Mchezaji huyo anatia dosari sifa ya Klabu.
Tukio hilo la Suarez kumng’ata Ivanovic lilitokea kwenye Mechi ya BPL, Barclays Premier League, iliochezwa Anfield na Liverpool kutoka sare 2-2 na Chelsea huku Suarez akishika makusudi na Chelsea kupata Penati waliyofunga na ni yeye Suarez ndie alieisawazishia Liverpool katika Dakika za majeruhi.

 MATUKIO YA MAKALI YA SUAREZ KATIKA  SOKA LA DUNIA:
Novemba 2007
Akiwa Nahodha wa Ajax alifungiwa na Klabu yake baada ya kupigana na mwenzake Albert Luque wakati wa Haftaimu kwenye Mechi.
Julai 2010
Afrika na Dunia nzima itamkumbuka Suarez, ambae ni Mchezaji wa Uruguay, kwa kuikatili Ghana huko Afrika Kusini kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia alipoushika mpira kwa makusudi kwenye mstari wa goli dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza na kuwanyima Ghana goli la wazi la ushindi.
Kwa kitendo hicho, Suarez aliwashwa Kadi Nyekundu na Ghana kupewa penati lakini Asamoah Gyan, ambae aliwahi kuwa Ligi Kuu England na Timu ya Sunderland, alikosa kufunga penati hiyo.
Novemba 2010
Alipata Kifungo cha Mechi 7 akiwa huko Uholanzi  na Klabu ya Ajax baada ya kumng’ata meno Mchezaji wa PSV Eindhoven Otman Bakkal kwenye mechi ya Ligi huko Uholanzi.
Octoba 2011
Wakicheza na Everton, alivunga amechezewa faulo na Jack Rodwell na kujidondosha na Rodwell akapewa Kadi Nyekundu.
Octoba 2011
Suárez alimkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kufungiwa Mechi 7 na kupigwa Faini Pauni 40,000.
Decemba 2011
Akiwa kwenye mashitaka ya kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kabla hajahukumiwa alionekana kutoa ishara ya matusi kwa Mashabiki wa Fulham kitendo ambacho kilimpa Kifungo cha Mechi 1.
Februari 2012
Man United na Liverpool walikutana tena Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu tukio la Suarez kumkashifu Kibaguzi Evra na Suarez, bila kutarajiwa, aligoma kumpa mkono Evra.
October 2012
Alishangilia Goli lake kwa kujirusha mbele ya Meneja wa Everton, David Moyes, ambae kabla ya Mechi hiyo na Liverpool alitamka Wachezaji wadanganyifu kama Suarez wnaohadaa Marefa wanafanya Mashabiki waikatae Soka ya England.
Januari 2013
Alipoza mpira kwa mkono na kufunga Bao la ushindi kwa Liverpool kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP dhidi ya Timu ya Daraja la chini Mansfield.
Machi 2013
Akiichezea Nchi yake Uruguay kwenye Mechi ya Mchujo ya kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014, Suarez alionekana kumtandika ngumi Beki wa Chile Gonzalo Jara bila Refa kuona.
FIFA wanachunguza tukio hili.
  
RATIBA- BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE:
Jumatatu Aprili 22
[Saa 4 Usiku]
Man United v Aston Villa
MSIMAMO==BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
NA TIMU P GD PTS
1 Man Utd 33 40 81
2 Man City 33 29 68
3 Arsenal 34 30 63
4 Chelsea 33 31 62
5 Tottenham 33 17 61
6 Everton 34 13 56
7 Liverpool 34 19 51
8 West Brom 33 -1 45
9 Swansea 33 1 42
10 West Ham 34 -7 42
11 Fulham 34 -8 40
12 Southampton 34 -7 39
13 Norwich 34 -20 38
14 Sunderland 34 -7 37
15 Stoke 34 -11 37
16 Newcastle 34 -17 37
17 Aston Villa 33 -24 34
18 Wigan 33 -23 31
19 QPR 34 -27 24
20 Reading 34 -28 24

 YANGA INANAFASI KUBWA KUTWAA UBINGWA POINT 1 TU
Vinara wa ligi kuu vodacom tanzania bara yanga sasa imefikisha pointi 56 baada ya kuitandika bao 3-0 Jkt ruvu  wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 47 na waliobakisha Mechi 3.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MECHI WALIZOBAKISHA YANGA:
Mei 1: YANGA v COASTAL UNION [UWANJA wa TAIFA]
Mei 18: YANGA v SIMBA [UWANJA wa TAIFA]
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Lakini ikiwa Azam FC watatoa sare au kufungwa Mechi yao inayofuata huko Mkwakwani hapo Aprili 27 dhidi ya Coastal Union, basi Yanga watachukua Ubingwa bila ya kucheza Mechi yao inayofuata.
RATIBA:
Jumatano Aprili 24
African Lyon v JKT Ruvu
Alhamisi Aprili 25
Simba v Ruvu Shooting
Jumamosi Aprili 27
Coastal Union v Azam FC
Jumapili Aprili 28
Simba v Polisi Moro
MSIMAMO:
NA TIMU P W D L GD PTS
1 Yanga 24 17 5 2 31 56
2 Azam FC 23 14 5 4 22 47
3 Kagera Sugar 23 11 7 5 8 40
4 Simba SC 22 9 9 4 11 36
5 Mtibwa Sugar 24 9 9 6 3 36
6 Coastal Union 23 8 9 6 3 33
7 Ruvu Shooting 22 8 6 8 0 30
8 JKT Oljoro 24 7 7 10 -5 28
9 Prisons FC 24 6 8 10 -7 26
10 Mgambo Shooting 23 7 4 12 -7 25
11 JKT Ruvu 23 6 5 12 -18 23
12 Toto African 25 4 10 11 -12 22
13 Police M 23 3 10 10 -10 19
14 African Lyon 23 5 4 14 -19 19