Wednesday, May 8, 2013

TIMU YA TAIFA YA BRAZIL KUZINDUA UWANJA WA MARICANA .

TIMU ya taifa ya Brazil inatarajiwa kuzindua rasmi uwanja wake uliokuwa katika matengenezo wa Maricana wakati watakapoikarinisha Uingereza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwezi ujao. Mapema ilifahamika kuwa kabla ya mchezo huo kungekuwa na mechi ya majaribio Mei 15 lakini halmashauri ya jiji la Rio de Janeiro liliahirisha mchezo huo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi. Uwanja huo ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho baadae mwezi ujao na Kombe la Dunia 2014 ulifunguliwa mwishoni mwa mwezi jana huku ukiwa umechelewa kwa miezi minne. Mechi baina ya Brazil na Uingereza mbayo itahezwa Juni 2 mwaka huu katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 78,000 ndio itakuwa pekee kabla uwanja huo haujatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho kuanzia Juni 15 hadi 30 mwaka huu. Ukarabati wa uwanja huo ambao umewahi kuweka historia ya kuingiza watu wengi zaidi wanaofikia 199, 858 katika mchezo wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 1950, umegharimu kiasi cha dola milioni 448 huku ukipunguzwa na kuwa na uwezo wa kuingiza watu 78,838 kwasasa.

FERGUSONA ATANGAZA RASMI KUTAAFU OLD TRAFORD


SIR ALEX FERGUSON Meneja wa klabu ya Manchester United,anatarajia kustaafu kuinoa klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu Katika mechi ya mwisho ya BPL dhidi ya West Bromich albion mei 18 mwaka huu baada ya kuifundisha kwa kipindi cha miaka 26 yenye mafanikio makubwa. Ferguson raia wa Scottland mwenye umri wa miaka 71 ameshinda mataji 38 tok alipochukua mikoba ya Ron Atkinson Novemba 1986, likiwemo taji la Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu. Mataji hayo yanajumuisha 13 ya ligi, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, matano ya Kombe la FA na manne ya Kombe la Ligi. 
Ferguson amesema uamuzi huo wa kustaafu ni uamuzi ambao ameufikiria kwa kipindi kirefu na kujiridhisha kwamba sasa ni muda muafaka wa kufanya hivyo. Kocha huyo amesema amesema ilikuwa ni muhimu kwake kustaafu huku akiiacha klabu hiyo ikiwa imara na anaamini amefanya hivyo na anategemea itaendelea kuwa juu kwa kipindi kirefu kijacho kutokana na damu changa atakazoziacha.

FERGUSON-MATAJI YAKE:
-PREMIER LEAGUE: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999,
2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.
-FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
-LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
-UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 1999, 2008
-UEFA CUP WINNERS CUP: 1991
-FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
-UEFA SUPER CUP: 1992
-FIFA INTER-CONTINENTAL  CUP: 1999
-FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011

Tuesday, May 7, 2013

IFAHAMU KWAUZURI TP MAZEMBE KATIKA ULIMWENGU WA SOKA:

Logo
TP MAZAEMBE

JINA KAMILI: Tout Puissant Mazembe
JINA LA UTANI:  (Kunguru)
KUANZISHWA MWAKA:1939 kama FC Saint-Georges
UWANJA :TP Mazembe, Lubumbashi
WAZAMAJI: {uwezo: 18,500)
RAISI: Moise Katumbi Chapwe
MENEJA:Lamine N'Diaye
LIGI: Linafoot


KOMBE LA MABINGWA VILABU / CAF LIGI YA MABINGWA:
Washindi (4): 1967, 1968, 2009, 2010
Runners-up (2): 1969, 1970
Kombe la Afrika la Washindi:
Washindi (1): 1980
CAF Super Cup:
Washindi (2): 2010, 2011
LIGI KUU KONGO MAARUFU LINAFOOT:
Washindi (12): 1966, 1967, 1969, 1976, 1987, 2000, 2001, 2006, 2007, 2009, 2011, 2012
Coupe du Congo:
Washindi (5): 1966, 1967, 1976, 1979, 2000
Runners-up (1): 2003
FIFA Kombe la Dunia:
Runners-up (1): 2010
UTENDAJI KATIKA MASHINDANO YA CAF
CAF Ligi ya Mabingwa: 10 kuonekana
2001 - Hatua ya Group
2002 - Nusu Fainali
2005 - Raundi ya mchujo
2007 - Raundi ya Pili
2008 - Hatua ya Group
2009 - Bingwa
2010 - Bingwa
2011 - hastahili katika hatua Group
2012 - Nusu Fainali
2013 - katika maendeleo
KOMBE LA MABINGWA WA KLABU: 7 KUONEKANA
1967 - Bingwa
1968 - Bingwa
1969 - Walifika fainali
1970 - Walifika fainali
1972 - Nusu Fainali
1977 - Raundi ya kwanza
1988 - Raundi ya kwanza
KOMBE LA SHIRIKISHO LA CAF: 3 KUONEKANA
2004 - Raundi ya kwanza
2006 - hastahili katika raundi ya kwanza
2007 - Hatua ya Group
KOMBE LA CAF LA WASHINDI: 2 KUONEKANA
1980 - Bingwa
1981 - Raundi ya Pili
CAF KOMBE: 1 KUONEKANA
2000 - Raundi ya Pili
CAF SUPER CUP: 2 KUONEKANA
2010 - Bingwa
2011 - Bingwa

FIFA YAMUWEKA MJUMBE MWINGINE PEMBENI


SHIRIKISHO la kandanda Duniani-FIFA limeendelea kujisafisha taratibu baada ya mjumbe wake wa kamati ya utendaji Chuck Blazer kusimamishwa jana ikiwa ni chini ya mwezi mmoja baada ya kutuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha akiwa kama katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la nchi za Amerika Kaskazini, Kusini na Carribean-CONCACAF. Blazer mwenye umri wa miaka 68 raia wa Marekani ambaye ilikuwa aachie nafasi hiyo ya kamati ya utendaji Mei 30 amesimamishwa na kamati ya maadili ya FIFA. Shirikisho hilo limedai kuwa wamefikia uamuzi huo kwasababu Blazer ameonekana kukiuka sheria mbalimbali za maadili za FIFA. Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya mjumbe mwingine wa kamati ya utendaji wa FIFA Vernon Manilal Fernando wa Sri Lanka kufungiwa miaka nane kwa kosa la ukiukwaji wa maadili.

CAF YATOA RATIBA KAMILI YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA


KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo inajivunia washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu itamenyana na Liga Maculmana ya Msumbiji kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo inafuatia upangwaji wa droo ya hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, inayodhaminiwa na Orange mjini Cairo, Misri leo. Katika droo hiyo, AS FAR Rabat ya Morocco iliyoitoa Azam FC katika Kombe la Shirikisho imepangwa kukutana na wapinzani wao, FUS Rabat. Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani aliongoza droo hiyo kwa pamoja na wawakilishi wa baadhi ya klabu zinazoshiriki michuano hiyo. Klabu nane zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa, St George, CA Bizerte, TP Mazembe, Enugu Rangers, JSM Bejaia, FUS Rabat, Stade Malien na Entente Setif zimeingia kwenye mbio za kuwania kurithi taji la AC Leopards ya Kongo, mabingwa wa Kombe la Shirikisho na mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu wakati marudiano yatakuwa kati ya Mei 31 , Juni 1 na 2. Mazembe ambao ni mabingwa mara nne Afrika, walitolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakifungwa 3-1 Afrika Kusini na kushinda 1-0 nyumbani.

DROO KAMILI YA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Stade Malien (Mali) vs Lydia (Burundi)
Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia)
FUS Rabat ( Morocco) vs ASFAR (Morocco)
CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri)
E.S Setif ( Algeria) vs US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia)
TP Mazembe (DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji)
St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri) 

MOTO KUWAKA CHELSEA KUUMANA NA TOTTENHAM KESHO"

Kona ya Charlie Adam katika Dakika ya 9 imezaa bao liliofungwa na Jon Walters baada ya hapo Sunderland walipata pigo baada ya mchezaji wake Craig Gardner kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kucheza rafu mbaya kwa Charlie Adam  katika dakika ya 63Sunderland walisawazisha kufuatia Frikiki ya Sebastian Larsson nakunaswa na  Nahodha John O’Shea alieachia Shuti na kutinga wavuni na kuwa Balake la pili tangu ahamie Sunderland kutoka Manchester United.
hivyo Sare hii imewafanya Sunderland wapande hadi nafasi ya 15 wakiwa Pointi 3 mbele ya Wigan walio nafasi ya 18 ambayo ndio moja ya Timu tatu za mwisho zinazoporomoka Daraja mwishoni mwa Msimu.
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA KESHO
Jumanne Mei 7
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Man City v West Brom
Wigan v Swansea
Jumatano Mei 8
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Tottenham

TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
36
42
85
2
Man City
35
30
72
3
Chelsea
35
34
68
4
Arsenal
36
31
67
5
Tottenham
35
18
65
6
Everton
36
14
60
7
Liverpool
36
25
55
8
West Brom
35
1
48
9
Swansea
35
-1
43
10
West Ham
36
-8
43
11
Stoke
36
-10
41
12
Fulham
36
-11
40
13
Aston Villa
36
-21
40
14
Southampton
36
-11
39
15
Sunderland
36
-12
38
16
Norwich
36
-22
38
17
Newcastle
36
-23
38
18
Wigan
35
-22
35
19
Reading
36
-26
28
20
QPR
37
-29
25
                            Hawa tayari wameshuka daraja  QPR & READING 

RED COAST, KARIAKOO, SAIGONI KUANZIA NYUMBANI RC

Upangaji ratiba (draw) ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) umefanyika leo (Mei 7 mwaka huu) huku mabingwa wa mikoa ya Dar es Salaam (Red Coast), Lindi (Kariakoo) na Kigoma (Saigoni) wakianzia nyumbani katika ligi hiyo itakayoanza Mei 11 au 12 mwaka huu.


Ligi hiyo itachezwa kwa mtoano kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ambapo mwenyeji atapanga tarehe ya mechi ambazo zinatakiwa kuchezwa kati ya Jumamosi au Jumapili. Mechi za marudiano katika raundi hiyo ya kwanza zitachezwa kati ya Mei 18 na 19 mwaka huu.

Katika upangaji huo ulioshuhudiwa na waandishi wa habari kwa niaba ya klabu husika, mabingwa wa Mkoa wa Shinyanga (Stand Ngaya FC) wamepita moja kwa moja hadi raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 25 na 25 mwaka huu wakati mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

Raundi ya tatu itachezwa kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati marudiano ni Juni 15 au 16 mwaka huu. Raundi ya nne itachezwa kati ya Juni 22 au 23 mwaka huu wakati marudiano ni Juni 29 au 30 mwaka huu. Raundi ya tano ni kati ya Julai 6 na 7 mwaka huu na marudiano ni Julai 13 au 14 mwaka huu.

Timu tatu ndizo zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao, ambazo ni ya kwanza nay a pili wakati timu ya tatu itapatikana kwa timu zilizoshindwa hatua ya nusu fainali kucheza zenyewe kwa zenyewe. Washindi wa nusu fainali nao watacheza wenyewe kwa wenyewe ili kupata bingwa wa RCL ambaye atakabidhiwa kombe la ubingwa.

Ligi hiyo inashirikisha mabingwa kutoka mikoa 27 ya kimpira ambapo katika raundi ya kwanza wanaanza mabingwa 26, raundi ya pili ni mabingwa 14 wakijumuisha na bingwa wa Shinyanga ambaye katika draw ameingia moja kwa moja katika hatua hiyo.

Raundi ya tatu itashirikisha timu saba zilizosonga mbele pamoja na moja yenye uwiano mzuri wa matokeo ili kufanya jumla ya timu nane. Raundi ya nne itakuwa na timu nne. Wakati raundi ya tano itakuwa ni kumpata bingwa na mshindi wa tatu.

Katika upangaji huo wa ratiba mechi za raundi ya kwanza (timu ya kwanza ikianzia nyumbani) itakuwa kama ifuatavyo; Red Coast vs Abajalo, Kariakoo vs Mtwara, Friends Rangers vs Kiluvya United,  TECKFOLT FC vs African Sports, Machava FC vs Flamingo SC, Gunners United vs Manyara na Simiyu vs Magic Pressure FC.

Nyingine ni Polisi Jamii Bunda FC vs UDC FC, Geita vs Biharamulo SC, Saigoni SC vs Tabora, Katavi Warriors vs Rukwa United, Mji Njombe vs Mbinga United na Kimondo FC vs Iringa.

Mechi zitachezwa katika viwanja vya makao makuu ya mikoa, vinginevyo kuwepo na maombi rasmi ambayo yatakubaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

SIMBA, MGAMBO SHOOTING UWANJANI KESHO
Timu za Simba na Mgambo Shooting ya Tanga zinaumana kesho (Mei 8 mwaka huu) katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh. 20,000.

RUVU SHOOTING, SIMBA ZAINGIZA MIL 17
Mechi namba 111 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyochezwa juzi (Mei 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1 imeingiza sh. 17,700,000.

Watazamaji 3,163 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,485,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,700,000.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,901 na kuingiza sh. 14,505,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 28 na kuingiza sh. 560,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,772,416.50, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,063,449.90, Kamati ya Ligi sh. 1,063,449.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 531,724.95, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 206,781.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 206,781.93.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)