Wednesday, May 8, 2013

FERGUSONA ATANGAZA RASMI KUTAAFU OLD TRAFORD


SIR ALEX FERGUSON Meneja wa klabu ya Manchester United,anatarajia kustaafu kuinoa klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu Katika mechi ya mwisho ya BPL dhidi ya West Bromich albion mei 18 mwaka huu baada ya kuifundisha kwa kipindi cha miaka 26 yenye mafanikio makubwa. Ferguson raia wa Scottland mwenye umri wa miaka 71 ameshinda mataji 38 tok alipochukua mikoba ya Ron Atkinson Novemba 1986, likiwemo taji la Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu. Mataji hayo yanajumuisha 13 ya ligi, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, matano ya Kombe la FA na manne ya Kombe la Ligi. 
Ferguson amesema uamuzi huo wa kustaafu ni uamuzi ambao ameufikiria kwa kipindi kirefu na kujiridhisha kwamba sasa ni muda muafaka wa kufanya hivyo. Kocha huyo amesema amesema ilikuwa ni muhimu kwake kustaafu huku akiiacha klabu hiyo ikiwa imara na anaamini amefanya hivyo na anategemea itaendelea kuwa juu kwa kipindi kirefu kijacho kutokana na damu changa atakazoziacha.

FERGUSON-MATAJI YAKE:
-PREMIER LEAGUE: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999,
2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.
-FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
-LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
-UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 1999, 2008
-UEFA CUP WINNERS CUP: 1991
-FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
-UEFA SUPER CUP: 1992
-FIFA INTER-CONTINENTAL  CUP: 1999
-FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011