TIMU YA TAIFA YA BRAZIL KUZINDUA UWANJA WA MARICANA .
TIMU ya taifa ya Brazil
inatarajiwa kuzindua rasmi uwanja wake uliokuwa katika matengenezo wa
Maricana wakati watakapoikarinisha Uingereza katika mchezo wa kimataifa
wa kirafiki mwezi ujao. Mapema
ilifahamika kuwa kabla ya mchezo huo kungekuwa na mechi ya majaribio
Mei 15 lakini halmashauri ya jiji la Rio de Janeiro liliahirisha mchezo
huo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi. Uwanja
huo ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho baadae
mwezi ujao na Kombe la Dunia 2014 ulifunguliwa mwishoni mwa mwezi jana
huku ukiwa umechelewa kwa miezi minne. Mechi
baina ya Brazil na Uingereza mbayo itahezwa Juni 2 mwaka huu katika
uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 78,000 ndio itakuwa pekee
kabla uwanja huo haujatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la
Shirikisho kuanzia Juni 15 hadi 30 mwaka huu. Ukarabati
wa uwanja huo ambao umewahi kuweka historia ya kuingiza watu wengi
zaidi wanaofikia 199, 858 katika mchezo wa fainali za Kombe la Dunia
mwaka 1950, umegharimu kiasi cha dola milioni 448 huku ukipunguzwa na
kuwa na uwezo wa kuingiza watu 78,838 kwasasa.