WANDINGA wa Jangwani mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, kinatarajia kuingia kambini kesho kutwa Ijumaa
kwa lengo i ya kujiweka sawa na mechi dhidi ya watani wao Simba utakaopigwa Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, Mei 18.
Kwa
mujibu wa habari tulizofanikiwa kuzipata kutoka ndani ya klabu hiyo, bado haijaamuliwa mahali
timu itakapoweka machimbo lakin sehemu hizi zinatazamwa sana kati ya Zanzibar na Bagamoyo
mkoani Pwani.
Yanga
kwa sasa inaendelea kujiweka sawa katika dimba la uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola ulioko Mabibo
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mtanange wao dhidi ya watani wao wa jadi
simba sc mchezo utakaopigwa tarehe 18 mei 2013.
Vijana
hao wa Jangwani, wametwaa ubingwa msimu huu baada kufikisha pointi 57 ambazo
haziwezi kufikiwa na timu nyingine.