Wednesday, May 8, 2013

KASEJA ASEMA SIWEZI KUZUNGUMZA LOLOTE KUHUSU MSIMBAZI

BAADA ya kuhusishwa na kuhamia katika klabu ya Ashanti, ambayo imepanda kucheza Ligi Kuu msimu ujao, Kipa namba moja wa timu ya Simba na ile ya Taifa, Juma Kaseja amesema ataweka wazi ni wapi ataenda baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu Kaseja amesema, ni mapema kuzungumzia hilo kwani ligi bado haijamalizika, ila atafanya hivyo mara tu ligi itakapomalizika.

 
Mkataba wangu unaisha mwezi Juni, hivyo wapenzi na mashabiki wangu kwa sasa watataka kujua nafanya nini, nawaahidi watajua hilo ligi itakapomalizika wakati mkataba wangu pia ukielekea ukingoni.
 
Kaseja amesema Mimi kama mchezaji nina malengo yangu, wasipate tabu nitasema mwenyewe na mtajua tu nini natarajia kufanya.
Aidha Kaseja kwa sasa ni mmoja wa wachezaji wakongwe hapa nchini na kutumainiwa katika kikosi cha Simba, na ameitumikia kwa mafanikio makubwa.

Hata hivyo mchezaji huyo alishawahi kufanya maamuzi magumu, kwa kuhamia kwa mahasimu wakubwa wa Simba, timu ya Yanga ambapo alicheza kwa msimu mmoja.