Friday, May 10, 2013

YANGA CHATUA VISIWANI PEMBA KUJIWEKA SAWA KUFUTA KIPIGO CHA 5-0

Wanandinga wa jangwani  Yanga SC wamewasili kisiwani Pemba kuweka kambi ya kujiandaa na mtanange mkali dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC Mei 18,  katika dimba la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
wanajangwani hao watakuwa huko hadi siku moja kabla ya mechi itakaporejea  jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwa  Yanga tayari imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu, lakini imeipa uzito mkubwa mechi hiyo kwa sababu inataka kulipa kisasi cha kufungwa 5-0 na wapinzani wao hao wa jadi mwaka jana.
Tangu utawala mpya  uingia madarakani, uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji umekuwa ukiumia kichwa na kipigo cha 5-0 mwaka jana.

Mara kadhaa Manji amewahi kukaririwa  akisema kwamba 5-0 zinamuumiza kichwa hasa katika wakati ambao idadi ya mabao katika mechi za timu hiyo ilipungua.
Kihistoria, Simba SC imewahi kuipa Yanga vipigo viwili vitakatifu 6-0 mwaka 1977 na 5-0 mwaka jana, wakati Yanga iliifunga SImba 5-0 mwaka 1969.  
Safari hii, Yanga imepania kuweka heshima kwa kuhakikisha inaitwangwa simba kwa  kipigo kitakatifu  na kuvunja rekodi ya 6-0 ya vipigo hivyo.


IFAHAMU KWA UNDANI ZAIDI YANGA KATIKA HARAKATI ZASOKA"

JINA KAMILI :Young  afrikani Sports Club
ILIANZISHWA : mwaka 1935
KOCHA: Ernie Brandts
LIGI: Ligi Kuu ya Tanzania bara
LIGI KUU TANZANIA:  Mara 24
1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011,2013
TANZANIA KOMBE  : Mara 4
1975, 1994, 1999, 2000.
CECAFA CLUB KOMBE / KAGAME INTERCLUB KOMBE:  Mara 5
Mwaka : 1975, 1993, 1999, 2011, 2012
UTENDAJI KATIKA MASHINDANO YA CAF   SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRIKA:
CAF LIGI YA MABINGWA: KUSHIRIKI  MARA 8
1997 - Raundi ya mchujo
1998 - Hatua ya makundi
2001 - Raundi ya Pili
2006 - Raundi ya mchujo
2007 - Raundi ya Pili
2009 - Raundi ya kwanza
2010 - Raundi ya mchujo
2012 - Raundi ya mchujo
KOMBE LA MABINGWA WA KLABU: 11 KUSHIRIKI
1969 - Robo Fainali
1970 - Robo Fainali
1971 - aliondoka katika raundi ya pili
1972 - Raundi ya kwanza
1973 - Raundi ya kwanza
1975 - Raundi ya Pili
1982 - Raundi ya Pili
1984 - Raundi ya kwanza
1988 - Raundi ya kwanza
1992 - Raundi ya kwanza
1996 - Raundi ya mchujo
KOMBE LA SHIRIKISHO LA CAF: 3 KUONEKANA
2007 – Raundi ya  mzunguuko wa  kati
2008 - Raundi ya kwanza
2011 - Raundi ya mchujo
CAF KOMBE: 2 KUONEKANA
1994 - Raundi ya kwanza
1999 - Raundi ya kwanza
Kombe la CAF la washindi: 2 kuonekana
1995 - Robo Fainali
2000 - Raundi ya kwanza

KAGERA SUGAR, SHOOTING KUUMANA KAITABA VPL

Kagera Sugar inaikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaofanyika kesho (Mei 11 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kaitba mjini Bukoba.

Ingawa timu zote mbili hazipambani kutafuta ubingwa ambao tayari umetwaliwa na Yanga wala kukwepa kushuka daraja, mechi hiyo bado ni muhimu kwao katika mazingira matatu tofauti.

Kagera Sugar inayonolewa na kocha mkongwe kuliko wote katika VPL, Abdallah Kibaden na ikiwa na pointi 40 yenyewe inasaka moja kati ya nafasi nne za juu ambazo zina zawadi kutoka mdhamini wa ligi, lakini pia timu zinazoshika nafasi hizo za juu zinapata tiketi ya kucheza michuano ya BancABC Super 8.

Kwa upande wa Ruvu Shooting ya Kocha Charles Boniface Mkwasa yenye pointi 31 inasaka moja ya nafasi sita za juu ambazo ni fursa ya kuingia kwenye Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) ambayo inatarajiwa kuundwa baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 28 mwaka huu.

Wagombea nafasi za uenyekiti na makamu wake ni lazima watoke katika timu zilizoshika nafasi sita la juu katika VPL msimu uliopita. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika siku moja kabla ya ule wa TFF uliopangwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.

Raundi ya 25 ya ligi hiyo itakamilika keshokutwa (Mei 12 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Mgambo Shooting ya Tanga. Mechi hiyo namba 169 itachezwa katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Azam yenye pointi 48 inahitaji moja zaidi ili kutetea nafasi yake ya umakamu bingwa iliyoutwaa msimu wa 2011/2013 na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Wakati Azam ikisaka pointi hiyo moja, Mgambo Shooting inayofundishwa na wachezaji wa zamani wa mabingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988, Mohamed Kampira akisaidiwa na Joseph Lazaro ni moja ya timu ziko katika hatari ya kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Mgambo Shooting inahitaji pointi moja tu katika mechi mbili ilizobakiza kukwepa kurudi FDL, ikishindwa kupata pointi hiyo huku Polisi Morogoro na Toto Africans ya Mwanza zikishinda mechi zao za mwisho kwa uwiano mzuri wa mabao itakuwa imekwenda na maji.

Mechi ya Azam dhidi ya Mgambo Shooting itachezeshwa na refa Jacob Adongo kutoka Mara, na atasaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Charles Mbilinyi wa Mwanza. Mwamuzi wa mezani atakuwa Idd Lila wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Omari Walii wa Arusha.

SIMBA, MGAMBO SHOOTING ZAINGIZA MIL 16
Mechi namba 149 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mgambo Shooting iliyochezwa juzi (Mei 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 imeingiza sh. 16,651,000.

Watazamaji 3,006 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,226,125 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,539,983.05.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,640,402.54, tiketi sh. 3,175,000, gharama za mechi sh. 984,241.53, Kamati ya Ligi sh. 984,241.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 492,120.76 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 382,760.60.

TFF YATAKA MAELEZO YA BARUA YA FIFA KWA DAUDA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti yawww.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Thursday, May 9, 2013

TIMU YA TAIFA CAMEROON SOON YAJA NA KOCHA MPYA


SHIRIKISHO la Soka nchini Cameroon-Fecafoot limetangaza kuwa tayari limechuja na kupata orodha ya majina mataji ya makocha watatu ambao mmoja wao atapewa jukumu la kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Indomitable Lions. Fecafoot wamepanga kutaja jina la kocha mpya atakayechukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa nchi hiyo Jean Paul Akono kabla ya mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia Juni mwaka huu. Akihojiwa rais wa Fecafoot Iya Mohammed alithibitisha kuteua majina matatu ambayo hakutaka kuyataja lakini amesema bado hawajateua jina rasmi la atakaekuwa kocha mpya wa nchi hiyo ingawa aliwaondoa hofu mashabiki wa soka watu kwamba hatua waliyofikia ni nzuri mpaka sasa. Pamoja na Mohammed kutoweka wazi majina ya walioingia tatu bora lakini kumekuwa na tetesi zimezagaa kuwa miongoni mwa makocha waliomo katika orodha hiyo ni pamoja na Raymond Domenech, Sven-Goran Eriksson na Volker Finke.

SIMBA YAINGIA MAKUBALIANO NA OCB LENGO KUU KUANDAA MKATI WA CLUB

WEKUNDU wa msimba  simba Sports Club inapenda kuwataarifu wanachama na mashabiki wake kwamba imeingia makubaliano na Open University Consultancy Bureau (Hapa itafaamika kama “OCB”) kwa ajili ya kuandaa mpango mkakati wa klabu (strategic plan).
Mchakato huo unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na makamu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-

1. Kuhusu makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.

2.  Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)

3. Kupitia mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.


Katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013   Referal Committee ya Simba Sports Club iliyochaguliwa ni:-


1. Joseph Itang’are

2. Swedy Mkwabi

3. Francis Waya

4. Ramesh Patel
5. Evance Aveva
6. Mulamu Ng’hambi
7. Salim Mhene
8. Mtemi Ramadhani
9. Moses Basena
10. Henry Tandau
11. Omary Gumbo
12. Michael Wambura
13. Glory Nghayomah
14. Crensencius Magori
15. Honest Njau
16. Ruge Mtahaba
17. Evodius Mtawala
18. Dr Mwafyenga


Kikao cha kwanza kati ya OCB na Kamati husika kitakuwa siku ya tarehe 25/5/2013.

Uongozi wa Simba Sports Club unawataarifu wanachama na wadau kwamba, mpango mkakati huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kujiendesha kiweledi (professionalism) kwani utabainisha malengo ya klabu kwa kipindi maalumu yakiwemo masuala muhimu kama ujenzi wa uwanja, academy set up, miundo mbinu ya klabu, masuala ya biashara za klabu yakilenga kukuza taswira (brand) ili kufanikisha mauzo ya bidhaa zenye nembo ya klabu, malengo ya mafanikio ya ndani ya uwanja, kujiwekea kiwango/kipimo cha utendaji wa klabu na wanachama (brand goodwill) ili kuvutia wawekezaji.

Mpango mkakati huo pamoja na hayo pia utaweka mipango hiyo katika uhalisia wa utekelezaji na muda wa kutekeleza masuala hayo, jambo litakalofanikisha kuleta kipimo cha utendaji wa uongozi na watendaji wa klabu katika uwajibikaji kwa wadau na wanachama wa klabu.

Mpango mkakati huo utakuwa tiyari kwa ajili ya kuingizwa katika mkutano mkuu wa klabu wa mwaka 2013/2014.
Imetolewa na 
Evodius Mtawala

Katibu Mkuu,

Simba Sports Club. 
9/5/2013

KOCHA WA TP MAZAEMBE ATIMULIWA WADHAFA WAKE"

KOCHA wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC, Lamine Ndiaye amejiuzulu wadhifa wake huo baada ya timu hiyo kuenguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Rais wa Mazembe, Moise Katumbi alitangaza kujiuzulu kwa kocha huyo na kudai kuwa na kudai kuwa wanafanya kila wawezalo ili kujaribu kuziba nafasi yake haraka iwezekanavyo. Katumbi amesema Ndiaye ameonyesha kuathiriwa na matokeo ya timu iliyoyapata katika ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na matatizo mengine ya ndani ndiyo maana ameamua kujiuzulu wadhifa wake. Hata hivyo Katumbi pamoja na kupokea barua hiyo ya Ndiaye lakini alimkatalia na kumpa nafasi ya kuendelea kufanya kazi ndani ya klabu hiyo. Ndiaye alitua Mazembe mwaka 2010 na kuingoza klabu hiyo kunyakuwa taji la ligi ya Mabingwa ya Afrika, mataji mawili ya Linafoot na kuifikisha timu hiyo katika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia. Wakati mchakato wa kupata mbadala wake ukiendelea makocha wa muda Pamphile Mihayo, David Mwakasu, Florian Mulot na Mandiaty Fall ndio watachukua jukumu la kuinoa timu hiyo yenye maskani yake jijini Lubumbashi kwa muda.

MFAHAMU DAVID MOYES KATIKA HARAKATI ZA SOKA NA UKOCHA

             DAVID MOYES
Jina kamili
David William Moyes
Kuzaliwa
25 April 1963 (age 50)
Alipozaliwa
Height
1.85 m (6 ft 1 in)
Nafasi
Sentahafu
TIMU 
Current club
TIMU ZA VIJANA ACADEMI
1978
1978–1980
TIMU ZA UKUBWA
Mwaka
Timu
mechi
{Goli
1980–1983
24
(0)
1983–1985
79
(1)
1985–1987
83
(6)
1987–1990
96
(11)
1990–1993
105
(13)
1993
5
(0)
1993–1999
143
(15)
Total
535
(46)
UKOCHA
1998–2002
2002–2013
2013–

MATAJI ALIOTWAA AKIWA NA CLUB
Celtic
Scottland Ligi Kuu (1): 1981-82
Bristol City
Kombe la Kiingereza Mshiriki Wanachama '(1): 1986
Preston North End
Ligi ya soka ya  daraja la Tatu  (1): 1995-1996
meneja.

TUZO BINAFSI ALIZOTWAA.
1.Lma Meneja wa Mwaka (3): 2002-03, 2004-05, 2008-09
2.Ligi Kuu  Meneja wa Mwezi (10): Novemba 2002, Septemba 2004, Januari 2006, Februari 2008, Februari 2009, Januari 2010, Machi 2010, Oktoba 2010, Septemba 2012, Mac 2013