TIMU YA TAIFA CAMEROON SOON YAJA NA KOCHA MPYA
SHIRIKISHO la Soka nchini Cameroon-Fecafoot limetangaza kuwa tayari limechuja na kupata orodha ya majina mataji ya makocha watatu ambao mmoja wao atapewa jukumu la kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Indomitable Lions. Fecafoot wamepanga kutaja jina la kocha mpya atakayechukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa nchi hiyo Jean Paul Akono kabla ya mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia Juni mwaka huu. Akihojiwa rais wa Fecafoot Iya Mohammed alithibitisha kuteua majina matatu ambayo hakutaka kuyataja lakini amesema bado hawajateua jina rasmi la atakaekuwa kocha mpya wa nchi hiyo ingawa aliwaondoa hofu mashabiki wa soka watu kwamba hatua waliyofikia ni nzuri mpaka sasa. Pamoja na Mohammed kutoweka wazi majina ya walioingia tatu bora lakini kumekuwa na tetesi zimezagaa kuwa miongoni mwa makocha waliomo katika orodha hiyo ni pamoja na Raymond Domenech, Sven-Goran Eriksson na Volker Finke.