Thursday, May 9, 2013

KOCHA WA TP MAZAEMBE ATIMULIWA WADHAFA WAKE"

KOCHA wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC, Lamine Ndiaye amejiuzulu wadhifa wake huo baada ya timu hiyo kuenguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Rais wa Mazembe, Moise Katumbi alitangaza kujiuzulu kwa kocha huyo na kudai kuwa na kudai kuwa wanafanya kila wawezalo ili kujaribu kuziba nafasi yake haraka iwezekanavyo. Katumbi amesema Ndiaye ameonyesha kuathiriwa na matokeo ya timu iliyoyapata katika ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na matatizo mengine ya ndani ndiyo maana ameamua kujiuzulu wadhifa wake. Hata hivyo Katumbi pamoja na kupokea barua hiyo ya Ndiaye lakini alimkatalia na kumpa nafasi ya kuendelea kufanya kazi ndani ya klabu hiyo. Ndiaye alitua Mazembe mwaka 2010 na kuingoza klabu hiyo kunyakuwa taji la ligi ya Mabingwa ya Afrika, mataji mawili ya Linafoot na kuifikisha timu hiyo katika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia. Wakati mchakato wa kupata mbadala wake ukiendelea makocha wa muda Pamphile Mihayo, David Mwakasu, Florian Mulot na Mandiaty Fall ndio watachukua jukumu la kuinoa timu hiyo yenye maskani yake jijini Lubumbashi kwa muda.