Thursday, May 9, 2013

RASMI: DAVID MOYES NI MENEJA MAN UNITED

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson anatarajiwa kukaa kwa mara ya mwisho katika benchi la ufundi la Old Traford mwishoni mwa wiki wakati timu hiyo itakapoikaribisha Swansea City, baada ya kutangaza kustaafu mwishoni mwa msimu. Katika mchezo huo ambao badala ya kuwa wa furaha utakuwa na huzuni kidogo wakati kocha huyo akiaga, United itakabidhiwa rasmi Kombe la Ligi Kuu nchini Uingereza walilotwaa msimu huu. Ferguson mwenye umri wa miaka 71 ameiongoza United kwa kipindi cha miaka 26 na kuisaidia kutwaa mataji mengi yakiwemo 13 ya ligi, mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya, matano ya FA na manne ya Kombe la Ligi. Mashabiki ambao watakosa tiketi za kwenda kushuhudia mechi hiyo ya mwisho kwa Ferguson Old Traford watapata nafasi siku ya Jumatatu ijayo kushikana mkono na kumuaga wakati timu hiyo itakapofanya matembezi katika mitaa ya jiji la Manchester kutembeza kombe lao. 
Mbali na hilo hii leo BODI ya Klabu ya Manchester United imekubalina na kupitisha moja kwa  moja mapendekezo ya Sir Alex Ferguson kuwa David Moyes awe Meneja mpya wa Klabu hiyo na  kumpatia Mkataba wa Miaka 6 utakaoanza Julai 1.
Uteuzi huu unafuatia kutangaza kustaafu kwa Sir Alex Ferguson hapo jana baada ya kuiongoza man u kwa  Miaka 27 tangu Novemba 1986 lakini atabakia Klabuni hapo kama Mkurugenzi na Balozi.
maneno ya Sir Bobby Charlton alisema: "mara zote nimesema tunataka Meneja anaefuatia awe Mtu wa Man United wa kweli. Kwa David Moyes tuna ni Mtu anaeelewa vitu tunavyotaka kuifanya Klabu hii spesheli. Tumempata Mtu ambae atakaa kwa muda mrefu na kujenga Timu za baadae. Uimara hujenga mafanikio.
David Moyes amesema: “Ni heshima kubwa kuteuliwa kuwa Meneja anaefuatia wa Manchester United. Nimefurahi sana kwamba Sir Alex ndie alienipendekeza kwa kuniona nafaa kwa kazi hii. Ninaheshimu sana vitu vyote alivyofanya na kwa Klabu hii. Najua ni ngumu mno kufuata nyayo za Meneja Bora katika Historia lakini hii nafasi ya kuiongoza Manchester United si kitu kinachokuja kila mara na nangojea kwa hamu kuanza kazi hii.
David Moyes atatambulishwa rasmi kuwa Meneja wa Man United hapo baadae kwani bado rasmi ni Meneja wa Everton na Mkataba wake unamalizika Tarehe 30 Juni.