Saturday, May 11, 2013

MBIO za mcheza tenisi nyota Andy Murray kufukuzia taji la michuano ya wazi ya Madrid zilisimamishwa na Tomas Berdych katika mchezo wa robo fainali na kumuacha Rafael Nadal kuwa mchezaji pekee anayeshika nafasi za juu kubakia katika michuano hiyo. Murray ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora duniani alishindwa kutamba mbele ya Berdych ambaye ni raia wa Jamhuri ya Czech kwa kukubali kipigo cha 7-6 6-4 huku Nadal naye akipambana na kumfunga Mhispania mwenzake David Ferrer kwa 4-6 7-6 6-0. 

Federer ambaye anashika namba mbili kwa ubora alijikuta aking’olewa na Kei Nishikori wa Japan siku moja baada ya kinara wa orodha hizo Novak Djokovic naye kung’olewa na Grigor Dimitrov baada ya kupata maumivu ya kifundo cha mguu wa kulia kwenye mchezo huo. 

Nadal sasa atakwaana na Pablo Andujar ambaye naye ni raia wa Hispania baada ya kumuondosha mbabe wa Federer, Nishikori katika hatua ya robo fainali. Vinara wote wanne Djokovic, Federer, Murray na Nadal ambaye anashika na nne kwa ubora watakutana tena katika michuano ya michuano wazi ya Italia wiki mbili zijazo.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United, Robin van Persie amemshukuru Sir Alex Ferguson kwa kumsaidia kutimiza ndoto zake kwa kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu. Kufuatia uhamisho wake uliogharimu kiasi cha paundi milioni 24 kutoka Arsenal msimu uliopita, mabao 25 aliyofunga Van Persie mwenye umri wa miaka 29 msimu huu yameisaidia klabu hiyo kutwaa taji lake la 20 la ligi hiyo. Van Persie amesema imekuwa ni heshima kubwa kwake kufanya kazi chini Ferguson mwenye umri wa miaka 71 ambaye atastaafu rasmi mwishoni mwa msimu huu baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa muda wa miaka 26. Nyota huyo aliendelea kusema amesikitishwa na kitendo cha kocha huyo kuamua kustaafu lakini anafurahi kwamba amepata nafasi ya kipekee ya kufanya nae kazi na anamuombea heri yeye pamoja na familia yake.

MKONGWE WA CHELSEA LAMPARD APIGA 2 AVUNJA REKODI

Kwenye mechi ya BPL LEO g la Dakika ya 88 la Frank Lampar limeleta burudani zaidi kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa bao2-1 dhidi ya  Aston Villa Bao na hilo ni Bao lake la 203 kwa Chelsea akiwa ameivunja Rekodi ya Bobby Tambling ya Magoli 202 iliyowekwa kati ya 1959 na 1970.
Katika mchezo huu kila timu ilimaliza ikiwa Mtu 10 baada ya Ramires wa Chelsea na Christian Benteke kutolewa kwa Kadi Nyekundu.

wachezaji hawa Wote walipewa Kadi za Njano mbili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa Ramires kutolewa Dakika ya 45 na Benteke Dakika ya 58.
MAGOLI:

Aston Villa 1

Benteke Dakika ya 14

Chelsea 2
Lampard Dakika ya 61 & 88
BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE

RATIBA
Jumapili Mei 12

[Saa 9 na Nusu Mchana]

Stoke v Tottenham

[Saa 11 Jioni]

Everton v West Ham

Fulham v Liverpool

Norwich v West Brom

QPR v Newcastle

Sunderland v Southampton

[Saa 12 Jioni]

Man United v Swansea

Jumanne Mei 14

[Saa 3 Dak 45 Usiku]

Arsenal v Wigan

[Saa 4 Usiku]

Reading v Man City

Jumapili 19 Mei

MECHI ZA MWISHO ZA LIGI MSIMU HUU

[Saa 12 Jioni]

Chelsea v Everton

Liverpool v QPR

Man City v Norwich

Newcastle v Arsenal

Southampton v Stoke

Swansea v Fulham

Tottenham v Sunderland

West Brom v Man United

West Ham v Reading

Wigan v Aston Villa
MSIMAMO:  BPL
PositionTeamPlayedGoalDifferencePoints
No movement1Man Utd364285
No movement2Man City363175
No movement3Chelsea373572
No movement4Arsenal363167
No movement5Tottenham361866
No movement6Everton361460
No movement7Liverpool362555
No movement8West Brom36048
No movement9Swansea36046
No movement10West Ham36-843
No movement11Stoke36-1041
No movement12Fulham36-1140
No movement13Aston Villa37-2240
No movement14Southampton36-1139
No movement15Sunderland36-1238
No movement16Norwich36-2238
No movement17Newcastle36-2338
No movement18Wigan36-2335
No movement19Reading36-2628
No movement20QPR36-2825

FAINALI YA FA CUP DIMBANI MAN CITY VS WIGAN ATHLETIC LEO

FAINALI YA FA CUP  hii leo man city mabingwa wa BPL msimu uliopita, man city wanaingia dimbani huku wakikumbuka kupokonywa taji lao la BPL na man united, na kutolewa katika michuano ya  UEFA championz ligi  katika hatua za makundi hivyo wamebakisha FA CUP tu ambapo wataumana uso kwa uso na timu ngumu ya  wigan athletic ambayo ipo hatarini kushuka daraja endapo man city wataibuka na ushindi basi  watakuwa wamemnusuru Meneja wao Roberto Mancini.
Kwa upande Man City ni Fainali ya 10 ya FA CUP na kwa upande wa  Wigan ni Fainali ya 1 tangu Timu yao ianzishwe Mwaka 1932.
FAINALI FA CUP
MUDA: SAA 1 NA ROBO USIKU LEO
UWANJA: WEMBLEY
MAN CITY VS WIGAN ATHLETIC

HARAKATI HADI KUFIKA FAINALI.
WIGAN:
-Raundi ya 3: Wigan 1 Bournemouth 1 MARUDIANO :Bournemouth 0 Wigan 1
-Raundi ya 4: Macclesfield Town  0 Wigan 1
-Raundi ya 5: Huddersfield Town 1 Wigan 4
-Raundi ya 6: Everton 0 Wigan 3
-NUSU FAINALI [Wembley]: Millwall 0 Wigan 2
MAN CITY:
-Raundi ya 3: Man City 3 Watford 0
-Raundi ya 4: Stoke City 0 Man City 1
-Raundi ya 5: Man City 4 Leeds United 0
-Raundi ya 6: Man City 5 Barnsley 0
-NUSU FAINALI [Wembley]: Man City2 Chelsea 2
Ukitoa tathimini ya haraka haraka Kwa Man City hii ni Mechi rahisi kwa upande wao kutokana wanakutana na timu kibonde Wigan Athletic ambayo katika Ligi, BPL,Barclays Premier League ipo katika janga la  kushusuhwa Daraja.
Man city fa cup wametwaa mara 5 na hii ni  fainali mara 10
Mwaka 1904, 1934, 1956, 1969 na 2011.
Kwa upande wa  Man United wamekuwa Washindi wa Pili mara 4 katika FA CUP  ambapo ni  Miaka ya 1926, 1933, 1955 na 1981.
WOTE WAWILI MATOKEO MECHI ZAMWISHO:
2012/2013
17 Apr Man City 1 Wigan 0
28 Nov Wigan 0 Man City 2
2011/2012
16 Jan Wigan 0 Man City 1
10 Sep Man City 3 Wigan 0
2010/2011
05 Mar Man City 1 Wigan 1
19 Sep Wigan 0 Man City 2
2009/2010
29 Mar Man City 3 Wigan 0
18 Okt Wigan 1 Man City 1

TIMU MBILI ZAIDI ZAPETA LIGI YA MABINGWA MKOA "RCL"

WAKATI Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaanza kutimua vumbi keshokutwa (Mei 12 mwaka huu), timu mbili zinakwenda moja kwa moja raundi inayofuata baada ya mabingwa wa Pwani, Kiluvya United kuondolewa na mkoa wa Manyara kutowasilisha bingwa wake.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Mei 10 mwaka huu) imeiondoa Kiluvya United baada ya kubaini kuwa timu hiyo haikushiriki ligi ya mkoa wala wilaya msimu uliopita, hivyo kutokuwa na sifa ya kucheza Ligi ya Mkoa msimu huu.
Hivyo Friends Rangers ya Dar es Salaam iliyokuwa icheze na Kiluvya United na Mpwapwa Stars ya Dodoma iliyokuwa iwakabili mabingwa wa Manyara zinakwenda moja kwa moja raundi ya pili.
Timu nyingine iliyokwenda moja kwa moja raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 25 na 25 mwaka huu na mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu baada ya kupita kwenye upangaji ratiba ni mabingwa wa Shinyanga, Stand United FC.
Kamati hiyo iliyokutana chini ya uenyekiti wa Blassy Kiondo pia imeagiza viongozi wa mikoa ya Manyara na Pwani waandikiwe barua za onyo kwa kushindwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao.
Vilevile imesisitiza viwanja vitakavyotumika kwa mechi za RCL ni vya makao makuu ya mikoa tu, isipokuwa kwa Uwanja wa CCM Mkamba ulioko Ifakara, Morogoro ambao ulishakaguliwa na TFF, hivyo kutumika kwa michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu. Pia usajili unaotumika katika RCL ni ule ule wa ligi ya mkoa.
Mechi za Mei 12 mwaka huu zitakuwa kati ya Kariakoo ya Lindi dhidi ya Coast United ya Mtwara (Uwanja wa Ilulu), Techfort ya Morogoro vs African Sports ya Tanga (Uwanja wa CCM Mkamba), Machava FC ya Moshi vs Flamingo SC ya Arusha (Uwanja wa Ushirika), Simiyu United ya Simiyu vs Magic Pressure ya Singida (Uwanja wa Simiyu) na Polisi Jamii Bunda ya Mara vs UDC ya Mwanza (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume).
Polisi SC ya Geita vs Biharamulo FC ya Kagera (Uwanja wa Geita), Saigon FC ya Kigoma vs Milambo FC ya Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika), Katavi Warriors ya Katavi vs Rukwa United ya Rukwa (Uwanja wa Katavi), Njombe Mji ya Njombe vs Mbinga United ya Ruvuma (Uwanja wa Sabasaba) na Kimondo SC ya Mbeya dhidi ya 841 KJ FC ya Iringa (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi kati ya Red Coast na Abajalo itachezwa Mei 13 mwaka huu Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Mei 12 mwaka huu uwanja huo utatumika kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Mgambo Shooting.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)